Home BUSINESS TASAC YAJIPANGA KUHUDUMIA WAFANYABIASHARA, DIASPORA COMORO

TASAC YAJIPANGA KUHUDUMIA WAFANYABIASHARA, DIASPORA COMORO

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limejipanga kutatua changamoto za wadau wanaotumia usafiri wa njia ya maji wanaosafirisha mizigo baina ya Tanzania na Visiwa vya Comoros.

Akitoa
salamu za Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa Meli, Mhandisi Said Kaheneko katika Kliniki ya Diaspora nchini Comoros iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoros, amesema ushiriki wa TASAC utaleta matokeo chanya kwa kuwa wadau wa sekta ya usafiri majini watapata fursa ya kuelezea changangoto zao na Wawakilishi wa TASAC waliopo Comoros wataweza kukusanya na kutatua changamoto hizo ambazo zimewasilishwa.

“Timu ya watumishi wa TASAC kutoka Idara mbalimbali wanashiriki katika Kliniki na hii itakuwa ni fursa nzuri ya kuona namna ya kutatua changamoto za wadau wetu, kutoa elimu kuhusu masuala ya usalama wa vyombo, kutembelea bandari pamoja na kubadilishana Mawazo na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Majini ya hapa Comoro,” amesema Mha. Kaheneko.

Aidha amempongeza Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu kwa kuona umuhimu wa kuandaa Kliniki hii ambayo imejumuisha wadau mbalimbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi kuweza kukutana na kutatua changamoto zinazowakabilia diaspora pamoja na kuangalia fursa zilizopo katika nchi ya Comoros.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Comoros Mhe. Saidi Yakubu amewashukuru Wakuu wa Taasisi wote walioruhusu maafisa wao kushiriki katika Kliniki ya Diaspora na kutoa rai kwa Diaspora kutumia siku hizo tatu kuweza kufika katika Kliniki ili kuweza kupata huduma.

“Shukrani za kipekee naomba nizipeleke kwa wakuu wote wa Taasisi zilizofika hapa, kwa kuitikia wito na kukubali kutoa huduma kwa watanzania wanaoishi Comoro. Naamini ujio huu utasaidia wao kupata huduma na changamoto zao kutatuliwa kwa wakati” amesema Balozi Yakubu.

Ubalozi wa Tanzania nchini Comoros umeaandaa Kliniki hii maalum kwa Diaspora katika viwanja vya Bunge, Moroni kuanzia leo tarehe 3 hadi 6, Agosti, 2024 ambapo jumla ya Taasisi 17 zinashiriki na kutoa huduma katika Kliniki hiyo.

Previous articleCHUO CHA BENKI KUU NI KITOVU CHA MAADILI NA NIDHAMU SEKTA YA FEDHA
Next articleWANANCHI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA BUTE NANE-NANE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here