Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) alipofika kuzungumzia maonesho ya nne ya Kimataifa ya madini yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Geita mwezi Septemba Mwaka huu.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule na Mtangazaji wa TBC Victor Elia (kushoto) wakatia akijiandaa kuingia Studio za shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwaajili ya Kipindi maalum kinachohusu maonesho hayo leo Agosti 17,2021. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
DAR ES SALAAM.
katika kuelekea kwenye maonesho ya nne ya Kimataifa ya Teknologia ya Madini Serikali ya Mkoa wa Geita imesema kuwa imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wadau wa Sekta hiyo hususani wachimbaji wadogo wanapata fursa ya kujifunza teknologia mpya ili kuweza kuwasaidia katika shughuli zao.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule ameyasema hayo wakati wa ziara yake fupi katika Studio za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Jijini Dar es Salaam alipofika kuzungumzia Maonesho hayo na mikakati iliyopo ambapo amesema kuwa maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku kumi nakwamba kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania watakaokuja kuonyesha Teknologia mbalimbali za uchimbaji zitakazoweza kuwasaidia wachimbaji wadogo katika shughuli zao na kuweza kunufaikanazo na kuweza wasaidia katika shughuli zao.
“Kwa mara ya kwanza maonesho haya yanakwenda kufanyika kimataifa kwa maana sasa kutakuwa na mataifa mengine ambayo yatakuwa yanakuja kushiriki kwenye maonesho haya, lakini kuja kuleta technologia mpya kwaajili ya wachimbaji wadogo ambao wamekuwa na changamoto kubwa sana kwenye upande wa tekinoligia hivyo hicho kitu kitakuwa na tija sana kwao kwani ndio kitu kikubwa kinachohitajika kwa wachimbaji wadogo kwenye nchi yetu” Amesema RC Rosemary.
Aidha ameongeza kuwa katika maonesho hayo watu watapata fursa ya kuona kiwanda kikubwa cha (Geita Gold Refinery- GGR) ambacho kimeshakamilika ambacho kitakuwa kinasafisha dhahabu kwa hatua ya mwisho ambapo amesema kuwa kiwanda hicho kitafanyakazi kubwa ya kusafisha dhahabu na kuiwezesha Serikali kuweza kuuza dhahabu iliyosafishwa nakwamba huo ni ufahari mkubwa kwa Mkoa wa huo na Nchi kwa ujumla.
“Uwepo wa Kiwanda hiki ni fahari ya nchi yetu ya Tanzania mana tunatakiwa tuuze madini ama dhahabu ghafi lakini kwa mara ya kwanza Tanzania tumepata kiwanda hicho ambacho kimeshathibitishwa Duniani ambacho kitaweza kusafisha dhahabu ya kiwango cha mwisho cha ubora. Sasa faida yake ni kuwa nchi yetu itauza dhahabu ambayo imesafishwa tofauti na kuuza dhahabu ghafi kwahiyo kwetu sisi ni fahari kwa Mkoa wa Geita, lakini ni fahari kwa nchi yetu ya Tanzania” Ameongeza.
Kwa upande wake Mwakilishi wa wafanyabiashara kutoka Sekta Binafsi Mkoa wa Geita ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa maonesho hayo Mhandisi Mwita chacha Wambura amesema kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa wafanyabishara kuweza kushiriki kwenye maonesho hayo huku akisisitiza kuwa zipo faida nyingi watakazoweza kupata ikiwemo kuona na kujifunza teknolojia mbalimbali za uchimbaji.
Nae Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo James Chiragi amesema kuwa Serikali ya Mkoa imejipanga vizuri na imeweka utaratibu mzuri wa washiriki kupata fursa ya kushiriki na kuonyesha shughuli zao nakwamba maandalizi yanakwenda vizuri.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo ‘SEKTA YA MADINI KWA KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WATU’ yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 16 Mwaka huu na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Mjaliwa.