Home BUSINESS MAAFISA BIASHARA WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO YA MSINGI.

MAAFISA BIASHARA WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO YA MSINGI.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA ) Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Maafisa Biashara wa mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida yanayofanyika kwa wa siku tano jijini Dodoma.

Maafisa biashara kutoka mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida wakifuatilia mafunzo ya sheria ya leseni za biashara yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) yanayofanyika katika ukumbi wa JK convetion Centre jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Bw. Godfrey Nyaisa (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Biashara wa mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro mara baada ufunguzi wa mafunzo ya Sheria ya Leseni za Biashara yanayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa JK Convetion Centre Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Leseni wa BRELA Bw. Andrew Mkapa na kutosho kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni wa BRELA, Bw. Tawi Kilumile


Na: mwandishi Wetu, Dodoma.

Maafisa biashara nchini wametakiwa kutambua  kuwa jukumu lao kuu ni kuwezesha  ufanyaji wa biashara badala ya kuwa wakusanya mapatato shughuli ambayo ni sehemu tu ya kazi ambayo wanatakiwa kuifanya

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya sheria za leseni za biashara kwa maafisa biashara wa mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro, yanayofanyika jijni Dodoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa  amesema Maafisa Biashara wanapaswa kutumia sheria pia kutumia busara wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na kwamba ikiwa watazifunga biashara wasitarajie mfanyabiashara huyo kufanya biashara na badala yake watachangia kuua uchumi wa nchi.   

“Muepuke sana kufunga biashara, afisa biashara kazi yako kubwa ni kusimamia wafanyabiashara, ikiwa utaifunga biashara utasimamia watu gani, hii ina maana huwataki wafanyabiashara “, alisema Bw. Nyaisa na kuongeza  kuwa anatarajia kuwa mafunzo hayo yatasaidia kubadili fikra na mitizamo ya maafisa biashara na watendaji wengine wa serikali  na kuwa watoa huduma na msaada kwa wafanyabiashara, hivyo ni vema wakafuatilia mafunzo hayo vizuri ili watakaporudi katika vituo vyao vya kazi watumike kama chachu  ya uwekezaji, ukuaji na uanzishwaji wa biashara.   

Bwa. Nyaisa amesema, kila mmoja awe kipimo kwa kuwezesha watu kuanzisha na kufanya biashara ili ifikapo mwisho wa mwaka kila mmoja ajipime na kujihoji ni watu wangapi aliowawezesha kuanzisha biashara, wawafuate watu na kuwawezesha kuanzisha biashara na sio watu wawafuate wao  kutaka kuanzisha biashara na wasiwe watu wanaokimbiwa na wafanyabiashara.

Sambamba na hilo maafisa biashara hao wametakiwa kutoa huduma bora na kwa weledi  jambo ambalo litawezesha  wafanyabiashara walio wengi kurasimisha biashara kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ama taasisi mbalimbali za kifedha. 

Amesisitiza kuwa maafisa biashara wana jukumu la   kuwaelimisha wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kusajili biashara zao na kupata  leseni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa wafanyabiashara hao ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi. 

Amewataka wafanyabiashara kuondokana na dhana  kwamba gharama ya usajili wa majina ya biashara na makampuni   kubwa  jambo ambali si kweli kwani BRELA ni taasisi ya huduma na gharama zinazotozwa ni ndogo.  

Mwisho.

Previous articleMAGAZETI YA LEOBJ.NNE AGOSTI 17,2021
Next articleRC ROSEMARY: MAONESHO YA MADINI MWAKA HUU YATAONGEZA FURSA KWA WACHIMBAJI WADOGO GEITA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here