Home BUSINESS TIC YAENDELEA KUVUTIA UWEKEZAJI KUTOKA CHINA

TIC YAENDELEA KUVUTIA UWEKEZAJI KUTOKA CHINA

DAR ES SALAAM 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendelea kuvutia uwekezaji kutoka nchini China, kikiwa na lengo la kuvutia kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 3 sawa na Shilingi Trilioni 7 kwa mwaka kutoka taifa hilo.

Kati 2013 -2023 TIC imepata uwekezaji zaidi ya Dola za Marekani zaidi ya Bilioni 10 sawa Shilingi Trilioni 27 kutoka China, TIC imepata Dola Bilioni moja, Shilingi Trilioni 3 kila mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri ameeleza hayo wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano na Kampuni inatoa huduma za Kisheria ya Yingke (China) ambayo ina Wanasheria zaidi ya 55,000 ikitoa huduma kwa Wateja zaidi ya 1,500,000.

Teri ameeleza kuwa TIC itaendelea kuvutia uwekezaji kutoka China kwenye sekta mbalimbali lakini kipekee lengo likiwa kuvutia uwekezaji kwenye sekta za Madini na Utalii.

Kwa upande wake, Mwenyekikiti wa Bodi Kampuni ya Yingke Law Firm, Xiangrong Mei amesema kupitia mashirikiano hayo na TIC, wataendelea kuleta Wawezaji tofauti nchini Tanzania ili kuinua uwekezaji.

Vile vile, Kongamano hilo limekutanisha Wawekezaji na Makampuni zaidi 20 na wenzao wa nchini Tanzania.

Previous articleWAZIRI MKUU KUZINDUA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMUA LA WAPIGA KURA
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA MACHIFU CHAMWINO JIJINI DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here