Home BUSINESS BoT KUANZA KUTOA ELIMU YA FEDHA KUANZIA SHULE ZA MSINGI

BoT KUANZA KUTOA ELIMU YA FEDHA KUANZIA SHULE ZA MSINGI

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akifurahia jambo na watoto waliotembelea katika Banda la Benki hiyo katika Maonesho ya Biashara ya 48 ya Kimataifa (Sabasaba), yaliyomalizika rasmi Julai 13,2024 kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Na; Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kutoka elimu ya fedha na uchumi kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi ili kuwajengea uelewa wakiwa wadogo ikiwemo kutambua alama za usalama zilizopo katika noti.

Akizungumza kwenye mahojiano na waandishi wa habari kwenye kilele cha maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa  (Sabasaba), Meneja Uhusiano Benki kuu ya Tanzania,  Vicky Msina, amesema wanaamini elimu wanayoitoa kwa watoto inakwenda kuwajengea tabia njema na nidhamu ya fedha, nakwamba watakuwa mabalozi wazuri kwa watoto wenzao na wazazi wao wakiwaelimisha kwa lugha nyepesi.

“Tunataka kuwajengea uwezo katika masuala ya fedha na uchumi, na tunaamini wanaenda kuwa na ujuzi na uthubutu wakuweza kutambua alama za usalama zilizopo katika noti zetu’ amesema.

Amebainisha kuwa katika siku zijazo kutakuwa na mitaala maalumu ya kutoa elimu ya uchumi na fedha kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, nakwamba tayari mazungumzo na wizara ya elimu yalishafanyika ili kuwa na mtaala maalumu wa kutoa elimu hiyo.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki maonesho ya Sabasaba yaliyomalizika rasmi Julai 13 mwaka huu, wakitoa elimu kwa wananchi namna wanavyotekeleza majukumu yao ya Kibenki hususani inavyosimamia sekta ya fedha nchini, na masuala mengine ikiwemo sera za fedha, namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali na mifumo ya malipo ya Taifa.

Meneja Uhusiano wa BoT, Vicky Msina akitoa maelezo ya namna ya kutambua noti kwa watoto waliotembelea Banda la Benki hiyo, kwenye maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yaliyomalizika rasmi Julai 13,2024 kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Previous articleSTAMICO YAINADI VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI
Next articleRAIS SAMIA AFUNGUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA POLISI MKOA WA KATAVI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here