Home BUSINESS TUNAHAKIKISHA MATOKEO YA TAFITI ZETU YANAIFIKIA JAMII – Prof. LWOGA

TUNAHAKIKISHA MATOKEO YA TAFITI ZETU YANAIFIKIA JAMII – Prof. LWOGA

Na : Georgina Misama, CBE, Dar es Salaam

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Edda Tandi Lwoga amesema Chuo kinatumia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kuhakikisha elimu na matokeo ya tafiti zinazofanywa zinawafikia wananchi popote walipo ili wazitumie katika kuboresha biashara zao.

Prof. Lwoga aliongea hayo Julai 11, alipofanya mkutano mfupi na Waandishi wa Habari katika banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba) wakati akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua ni mikakati gani ambayo Chuo kimejiwekea katika kuhakikisha tafiti zake zinaifikia jamii.

“Mwaka huu tumeanzisha midahalo ya wazi (Public lectures) ambapo tunawashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya chuo, midahalo hiyo inaelimisha jamii kwenye fursa mbalimbali lakini pia tunaitumia kuwapa matokeo ya tafiti zetu, na zaidi tuhakikisha majadiliano hayo yanasambazwa kupitia mitandao ya kijamii ” alisema Prof. Lwoga.

Vilevile alisema Chuo kinafanya Kongamano la Kimataifa ifikapo mwezi Novemba kila mwaka, kongamano hilo linahudhuriwa na wafanyabishara pamoja na wadau mbalimbali katika Sekta ya Biashara na Uchumi ili kuwapa fursa ya kushiriki matokeo ya tafiti zinazofanywa na Chuo hicho.

“CBE pia ina utaratibu maalum wa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wajasiriamali na wafanyabishara mbalimbali ambapo pamoja na mafunzo hayo tunawasambazia pia matokea ya tafiti zetu ili wakishayapata wayaelewe na waweze kuyatumia katika kuboresha biashara zao.

Ikumbukwe ni miaka 60 sasa tangu CBE kianzishwe hii inafanya chuo Chuo hicho kikongwe kubobea katika masuala ya elimu ya biashara nchini, katika ushiriki wake sabasaba CBE kimeendelea kuonyesha huduma za elimu zinazopatikana chuoni hapo ikiwemo mafunzo ya muda mrefu na mfupi pamoja na matumizi ya mtandao katika kutoa elimu.

Previous articleWANANCHI MKALAMA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Next articleWAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA MNARA WA MASHUJAA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here