Na: Hughes Dugilo, Dar.
CHUO cha ufundi stadi cha Tehama VETA Kipawa chaa Jijini Dar es Salaam kimewataka vijana kimetoa rai kwa Watanzania hasa vijana kuhakikisha wanajiunga kwenye chuo hicho ili kusoma kozi ya ufundi wa simu za mkononi kwa lengo la kujiajiri na wakati huo huo kuongeza usalama kwa watumiaji wa simu hizo.
Akizungumza wakati wa mahojiano maalum kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa katika Banda la VETA Mratibu wa Miradi na Uzalishaji katika chuo hicho amesema kozi hiyo imeanzishwa kimkakati.
“Kozi ya ufundi wa simu ni ya kimkakati na ilianzishwa kwa lengo kuu kuongeza usalama kwa mtumiaji wa simu za mkononi.Sasa hivi simu ya mkononi imekuwa kila kitu kwa maisha ya watanzania na hata watu wengine duniani.
“Watumiaji wa simu kwao imekuwa ndio kila kitu, wanatumia kama sehemu ya mawasiliano lakini pia ni kifaa cha kuweza kufanya miamala ya kifedha.Pia wanatumia kama sehemu ya chanzo cha taarifa.
“Kwa hiyo watumiaji wengi wa simu za mkononi wamekuwa wakitumia simu zao kila siku na zimekuwa na taarifa nyingi mno za mtumiaji ambazo kwa muda mwingine zikitoka kwa mtu ambaye sio sahihi zinahatarisha usalama wa yule mtu,amesema Mapuli.
Amesema hivyo lengo la hiyo kozi ni kuongeza usalama wa mtumiaji wa simu za mkononi, pia kuweza kuchangia kwenye pato la taifa na uchumi kwa ujumla kwasababu ukiwa na simu ni nyenzo kiuchumi.
“Kwa hiyo chuo cha TEHAMA –VETA Kipawa tushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) tuanzisha hii kozi kimkakati tukiwa na lengo la kuongeza usalama na hadi sasa tumetoa mafunzo katika mikoa kadhaa.
“Baadhi ya mikoa hiyo ni Kigoma,Dodoma, Arusha, Tanga na Kilimanjaro kwa watu zaidi ya 500 kwenye kozi ya ufundi wa simu.Pia tumetoa mafunzo haya hapa chuoni kupitia mradi wa SDF kwa wanafunzi 4,700 kwa mwaka 2021 na tunaendelea kutoa mafunzo haya kwa watanzania wote.
“Kwa ujumla kila mwezi hii kozi inaanza na tunapokea maombi ya si chini ya watu 10 mkapa 20 ambao wanakuja kujifunza.Tunaamini mbali na kuongeza usalama kwa watumiaji wa simu.
“Lakini ni chanzo cha ajira kwa vijana, ufundi wa simu za mkononi umeajiri watu wengi sana, ukisoma kozi ya ufundi wa simu unahitaji mjati mdogo sana kuweza kujiajiri , kwa hiyo tunahamasisha vijana walioko mtaani wafike Chuo cha VETa Kipawa kujisajili,”amesema.
Amesisitiza ni vema vijana wajitokeza kwenye kozi hiyo ya ufundi wa simu waweze kujiajiri lakini pia kuchangia kwenye kuongeza usalama wa watumiaji wa simu za mkononi Tanzania.
Kwa upande wake Unice Kavishe ambaye ni mwanafunzi aliyejifunza mafunzo ya ufundi simu kupitia VETA Kipawa na sasa amejiajiri anafanya ufundi wake katika maeneo ya Mtaa wa Agrey na Masasi uliopo Kariakoo.
Amesema kabla ya mafunzo hayo walikuwa wanatengeza simu lakini mafundi wengi walikuwa wanaweza kutengeza simu lakini linatokea tatizo au ikatokea tofauti ya mazungumzo kati yao na wateja na hakukua na sehemu kupata haki.
“Kwasababu hakukua na chuo chochote cha kutoa haya mafunzo kwa hiyo Serikali iliamua kurasimisha kutoa haya mafunzo ili watu wafanye kazi kwa uweledi na umakini , tunaishukuru Serikali kwasababu baada ya haya mafunzo mafundi wengi waliopita VETA wanafanya kazi kwa ufasa na wamepunguza kesi zilizokuwa zinatokea”
“Tunaomba Serikali iendelee na haya mafunzo kwasababu watu wengi wanahitaji na kama mlivyo mkakati wa Serikali kuwa na viwanda tunahitaji kuwa na watu wanaoweza kufanya hizi kazi.”