Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani nchini (FCC) Bw. William Erio amefungua mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa tume hiyo yaliyoandaliwa na Novelty Analysis Consultants yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa mpana namna uendeshaji biashara na uchumi katika mtandao.
Akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo hayo leo Mei 15, 2024 jijini Dar es salaam Bw. Erio amesema yamelenga kwa watumishi hao kutokana na FCC ndio wasimamizi wa udhibiti wa mambo ya kiuchumi nchini hivyo kupitia mafunzo hayo yatalenga kuishauri serikali namna bora ya kuangalia uendeshaji wa biashara na uchumi katika masoko mtandao na sheria zipi zitungwe ili kumlinda mlaji na mtumiaji wa mwisho wa bidhaa husika.
Bw. Rafael Mazer mshauri kutoka Novelty Analysis Consultants akitoa mafunzo kwa watumishi wa vitengo mbalimbali kutoka FCC yenye lengo la kuwajengewa uwezo na uelewa mpana uendeshaji biashara na uchumi katika mtandao
Zaytun Kikula Mkurugenzi wa Tafiti, Miungano ya Kampuni na Uraghabishi Tume ya Ushindani FCC (kushoto)
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Kenya (CAK) na Mshauri kutoka Novelty Analysis Consultants Bw, Wang’ombe Kariuki akieleza jambo kwenye mafunzo kwa watumishi wa FCC.
Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio (wa pili kutoka kulia) akizungmza jambo wakati akifungua mafunza kwa watumishi wa FCC yanayolenga kuwajengewa uwezo na uelewa mpana kuhusu uendeshaji biashara na uchumi katika mtandao
Kwenye picha ya pamoja watumishi wa FCC waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Novelty Analysis Consultants
Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio (wa kwanza kulia), Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Kenya (CAK) na Mshauri kutoka Novelty Analysis Consultants Bw, Wang’ombe Kariuki (kushoto) pamoja na Bw. Rafael Mazer mshauri kutoka Novelty Analysis Consultants (katika)