Home BUSINESS BRELA KUSHIRIKIANA NA TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI KULETA UFANISI KWENYE MILIKI UBUNIFU

BRELA KUSHIRIKIANA NA TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI KULETA UFANISI KWENYE MILIKI UBUNIFU

Dar es Salaam

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wamesaini makubaliano na Taasisi Nne za Serikali ya kushirikiana ili kuleta ufanisi katika maeneo mbalimbali ya kibiashara hapa nchini.

Makubaliano hayo, yamefanyika leo Mei 9, 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu Jijini Dar es Salaam, ambapo Taasisi zilizotiliana saini na BRELA ni pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe, TIA na Mamlaka ya Afya ya Viwatilifu (TPHPA) .

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma  akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ameiagiza BRELA na COSOTA  kutoa elimu ya kutosha kwa wabunifu hapa nchini ili wanufuike na kazi zao.

“Niwaelekeze BRELA na COSOTA wakae Kwa pamoja waangalie namna ya kutoa elimu ya Miliki Ubunifu kwa wabunifu wakiwemo wasanii wachanga, ili wanufaike na kazi zao” amesema Mwinjuma.

Aidha ameongeza kuwa BRELA wanatakiwa kuhakikisha wanajielekeza kuifanya Miliki Ubunifu inatambulika, ili wabunifu waweze kukopesheka na kuendeleza kazi zao.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa, amesema elimu ya Miliki Ubunifu bado iko chini na kwamba Taasisi yake inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali katika sekta hiyo.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanafikia malengo yao, wamekuwa na utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wafanyakazi wao kujiendeleza na masomo katika fani ya Miliki Bunifu ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, Afisa Mtendaji Mkuu huyo na Naibu Waziri Mwinjuma, walikabidhi mfano wa hundi  wa Sh. Million 16.5 kwa kila mmoja, kwawanufaika wanne wa masomo ya Miliki Ubunifu.

Previous articleRAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MALORI CHA SATURN CORPORATION KIGAMBONI
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 10-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here