Home BUSINESS DKT. KIRUSWA – USALAMA MAHALA PA KAZI IWE KIPAUMBELE MIGODINI

DKT. KIRUSWA – USALAMA MAHALA PA KAZI IWE KIPAUMBELE MIGODINI

Imeelezwa kuwa, usalama mahala pa kazi ni jambo muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na wachimbaji wote wa madini nchini akiwemo mwajiri pamoja na waajiriwa, wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa.

Hayo, ameyabainishwa na Dkt. Kiruswa baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji na uchenjuaji madini ya dhahabu wa Maweni Gold Mine uliopo katika kijiji cha Maweni mkoani Manyara.

Dkt. Kiruswa amesema usalama katika shughuli za uchimbaji madini ni suala muhimu kuliko hata madini yanayochimbwa katika eneo husika ambapo amewataka waajiri na waajiriwa kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anajilinda na kuwalinda wengine.

Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amewapongeza wawekezaji katika mgodi huo na kuwataka kuzingatia Sheria za Madini ikiwemo kulipa kodi na tozo mbalimbali za serikali.

Naye, Kamshna wa Madini Dkt. Abdulrahiman Mwanga amemtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara Mhandisi Ernest Sanka kutoa semina na mafunzo mbalimbali kuhusu elimu ya usalama mahala pa kazi ili wafanye shughuli zao kwa usalama.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanga ameutaka uongozi wa kampuni ya Maweni Gold mine Ltd kuhakikisha unajenga mahusiano mazuri na jamii iyozunguka eneo wanalofanyia shughuli zao.

Naye, Meneja wa Maweni Gold Mine Ltd Emmanueli Maguzu amesema mgodi wao umefunguliwa rasmi tarehe 4 Julai na unatarajiwa kuzalisha kilo moja na nusu za dhahabu kwa mwezi.

Pia, Maguzu amesema kuwa, kwa sasa mgodi huo umeajiri wafanyakazi 20 upande wa uchenjuaji, wapishi wawili pamoja na walinzi 10 ambapo wanategemea kuajiri wafanyakazi wengi zaidi watakapoanza shughuli za uchimbaji ambapo kwa sasa wameanza shughuli za uchenjuaji pekee.

Previous articleMATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI YA MAJI YNAHITAJIKA KUKABILINA NA CHANGAMOTO YA MAJI KWENYE KILIMO
Next articleHABARI PICHA: DKT. MABULA ATEMBELEA BANDA LA TWCC, APONGEZA UBORA WA BIDHAA NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA WAJASIRIMALI SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here