Mhandisi Mchenjuaji, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mha. Happy Mbenyange akizungumza na vyombo vya Habari wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ziliyofanyika leo machi 8, 2024, katika wilaya ya kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAMÂ
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO ) wamefurahishwa na ushirikishwaji unaofanywa ndani ya Shirika hilo na mafanikio katika miradi yake.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Mchenjuaji kutoka STAMICO Mha. Happy Mbenyange wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ziliyofanyika machi 8, 2024, katika wilaya ya kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Mha. Mbenyange amesema wanawake wanauwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati moja na kwa umakini mkubwa, jambo lililothibitika kupitia mradi wa kuzalisha Nishati mbadala ya kupikia ya Rafiki Briquette
‘”Niipongeze sana Menejimenti ya STAMICO kwa kuwekeza kwa wanawake na kuwapa nafasi sawa na wanaume katika kusimamia miradi, jambo ambalo linatupa hamasa sisi wanawake kusimamia kwa bidii, ili kuondoa dhana ya uduni wa mwanamke katika kufanya kazi kwa ufanisi”
Ametoa rai kwa wanaume nchini kuendelea kutoa fursa na kuwasaidia wanawake kufikia malengo na mafanikio katika kazi mbalimbali wanazofanya.
Ametoa rai kwa wanaume nchini kuendelea kutoa fursa na kuwasaidia wanawake kufikia malengo na mafanikio katika kazi mbalimbali wanazofanya.
Amewasihi wanawake kujiamini, kujituma na kuonesha uwezo wao pindi wanapopata nafasi ya kutekeleza majukumu mbalimbali.
Aidha amewahamasisha watoto wakike kuchangamkia fursa za kitaaluma hususani katika nyanja za sayansi ili waweze kuongeza ushindani katika kazi za kihandisi.
STAMICO imeshiriki katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu kupitia ofisi zake za Dodoma, Dar es Salaam na Kiwira yakiwa na kauli mbiu ya ‘Wekeza kwa Wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na Jamii’