Home LOCAL WAZIRI MKUU AKAGUA MAENDELEO YA UWANJA WA NDEGE WA MUSOMA

WAZIRI MKUU AKAGUA MAENDELEO YA UWANJA WA NDEGE WA MUSOMA

1000615244
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa soko la kimkakati la Tarime mjini unaotarajiwa kugharimu sh. bilioni 9.6 hadi kukamilika kwake.
Akipokea taarifa ya ujenzi wa soko hilo jana jioni (Jumatano, Februari 28, 2024) Waziri Mkuu alielezwa kwamba mradi huo kwa sasa upo katika hatua ya umaliziaji na umefikia asilimia 82 ya utekelezaji.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa soko hilo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Tarime. “wilaya hii ni ya kimkakati kibiashara kwasababu imepakana na nchi jirani ya kenya na manunuzi yao wanayafanya hapa”
Akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime, Bi. Gimbana Ntavyo alisema shughuli zinazoendelea kwa sasa ni skimming, upakaji wa rangi, ufungaji wa milango kwenye maduka na vyoo na ufungaji wa mifumo ya umeme na maji kwenye jengo kuu la soko.

 

1000615351
Alisema kazi nyingine ni uwekaji wa vigae na terazo kwenye vizimba, maduka ya nje na ndani na kwa upande wa kazi za nje, wanaendelea na uzalishaji wa paving na kuandaa maeneo ya kuzipanga.
“Hadi sasa malipo yaliyofanyika kwa mkandarasi ni sh. bilioni 5.77 na kwa mshauri ni sh. milioni 120.36 sawa na asilimia 60.86 ya gharama za mradi,” alisema na kuongeza: “Mradi huu utakuwa na maduka 325, vizimba 160, mabucha matatu, migahawa miwili, supermarket moja na Benki mbili.”
Akielezea manufaa ya mradi huo, Mkurugenzi huyo alisema mradi huo umetoa ajira za muda kwa watu 441 na utakapokamilika, Halmashauri inatarajia kuongeza mapato yake ya ndani kwa sh. milioni 588 kwa mwaka kutokana na mapato yatakayokusanywa.
1000615350
1000615349
Previous articleRAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA UJUMBE WA KANISA LA KILUTHERI AFRIKA MASHARIKI (KKAM) IKULU ZANZIBAR
Next articleMIZIMU YA KATABI HIFADHI YA TAIFA KATAVI YAWAKIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here