Home BUSINESS MIZIMU YA KATABI HIFADHI YA TAIFA KATAVI YAWAKIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII.

MIZIMU YA KATABI HIFADHI YA TAIFA KATAVI YAWAKIVUTIO KIKUBWA CHA UTALII.

Na: Mwandishi Wetu _Katavi

IMEBAINISHWA kuwa Hifadhi ya Taifa Katavi ni moja ya Hifadhi ambayo inavivutio vingi vya utalii ikiwepo kivutio kikubwa cha ziwa katavi ambalo limebarikiwa kuwa na viboko wengine sana ukilinganisha na maeneo mengine .

Hayo yamebainishwa februari 28 ,2024 na Afisa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Katavi Beatrice Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo mkoani humo kwalengo la kuuzungumzia utalii wa hifadhi hiyo ya katavi.

Amesema kuwa Hifadhi ya taifa Katavi inasifika sana Kwa uwepo wa viboko wengi hasa kupitia ziwa katavi lakini licha ya kusifika na kuwa na viboko wengi kupitia ziwa katavi lakini Kuna vivutio vingine Kama wanyama mbalimbali .

Nawashauri watanzania kujenga utaratibu wa kudumu wa kutembelea vivutio vilivyopo katika Hifadhi yetu ya katavi na hasa nyakati kama vile watoto wapo katika mapumziko ,nivema kuja kuona.”Amesema

Akizungumzia kuhusu historia ya mkoa wa Katavi ,Afisa UHIFADHI Beatrice Amesema jina la katavi lilitokana na jina la Katabi ambaye alikuwa kama chifu na alikuwa anajishughuliaha mambo ya uwindani pamoja na kufanya matambiko mbalimbali ya kuomba mizimu Kwa lengo la kufanikisha jambo furani .

Amesema Katabi alikuwa ni kiongozi wa kimila katika mkoa huo ambapo jina lake la Katabi ndio umepatikana mkoa wa Katavi na Kwa wakati huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alikuwa anaingia pasipo kupata kibari cha Katabi mwenyewe.

“Kimsingi Kwa histoa mkoa wa Katavi umetokana na mtu ambaye aliitwa Katabi ,na alikuwa ni kiongozi wa kimila na shughuli zake kubwa ilikuwa ni uiwindaji na kufanya matambiko kupitia makabila ya wapimbwe na Wabende.”Amesema

Nakuongeza kuwa ” mahala hapo ambapo palikuwa panafanyiwa matambiko pamekuwa ni sehamu ya kivutio cha utalii na Kwa makabila yanayozunguka Hifadhi hii na mkoa wa Katavi Kwa ujumla bado wanaendelea kufanya ibada lakini Kwa kibari kutoka TANAPA .”Amesema

Amewahamasisha watanzania kuja kutembelea Hifadhi hiyo ya taifa ya katavi ili kujionea vivutio vilivyopo lakini pia wageni kutoka nje ya Tanzania ikiwa pamoja na Afrika Mashariki kuja kutazama ukubwa wa hifadhi hiyo ambayo iliazishwa mwaka 1974.

“Ndugu zangu watanzania zile nyakati za likizo njoo kwenye Hifadhi yetu ya katavi uje uone uzuri wake hakika utaona wanyama Kwa karibu na utajivunia kuwa sehemu ya mtalii kupitia Hifadhi hii.”Amesema .

Pia amesema Hifadhi ya katavi Ina utalii wa Maji meupe, uoto wa asili, hivyo watanzania wajitokeze kutembelea Hifadhi yao ya katavi kwakweli watafurahia madhari ya utalii iliyopo kwenye Hifadhi hiyo.

Previous articleWAZIRI MKUU AKAGUA MAENDELEO YA UWANJA WA NDEGE WA MUSOMA
Next articleRAIS SAMIA ATANGAZA KIFO CHA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI IKULU DAR ES SALAAM 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here