Waziri Kijaji ameyasema hayo jijini Dodoma wakati alipofanya ziara katika Viwanda vya kuzalisha mabati vya ALAF na Herosean Interprises inayozalisha mabati ya DRAGON ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na Viwanda hapa nchini zinanoreshwa.
Aidha Mhe. Waziri akiwa kwenye kiwanda cha Herosean Interprises kinachozalisha mabati ya DRAGON ameweza kubaini uwepo wa bidhaa nyingine ambazo haziusiani na malengo halisi ya leseni iliyotolewa na BRELA.
“Leo nimetembelea Viwanda hivi viwili lakini cha kusikitisha hiki Kiwanda cha kuzalisha mabati ya DRAGONI kinajihusisha na biashara ya kuuza bidhaa nyingine ikiwemo Friji, PVC, Vigae na Gypsum bord ,
“Nimewataka wanioneshe vielelezo vya usajili wa bidhaa hizo tofauti na bidhaa za mabati kiwandani hapa,sikupata majibu sahihi , naziagiza taasisi zinazohusika na hili suala zilishughurikie ili kupata ukweli wake. Amesema Kijaji
Vile vile Waziri Dkt.Kijaji ametoa wito kwa Viwanda vinavyozalisha bidhaa za mabati hapa nchini kuuzwa kwa bei rafiki ili kunufaisha wanunuaji kwa makundi yote.
”Jambo lingine ninalotaka kuwaambia watanzania kwa bidhaa nilizotembelea leo ,ukilinganisha kwa nchi za Afrika mashariki kwa bidhaa hii ya mabati sisi Tanzania bei yetu ipo chini kuliko nchi yoyote ile ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo niwatake msisikilize kelele za mtaani endeleeni kujenga kwa wingi na sisi kama Serikali tunaendelea kutekeleza miradi yetu”Ameongeza Dkt. Kijaji.
Kwa nyakati tofauti, wazalishaji wa viwanda hivyo Herry Jailos afsa huduma kwa wateja kiwanda cha mabati ya Alaf na Boniface Lekwasa Afsa Masoko Kiwanda cha kuzalisha mabati Dragon
wameishukuru Serikali kufanya ziara na kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa masoko kutokana na wazalishaji wa bidhaa hizo kuwa wengi nchini.