Home BUSINESS CHUO KIKUU MZUMBE KUWAINUA VIJANA NA WAJASIRIAMALI WADOGO KWA KUWAPATIA MITAJI KWA...

CHUO KIKUU MZUMBE KUWAINUA VIJANA NA WAJASIRIAMALI WADOGO KWA KUWAPATIA MITAJI KWA NJIA YA MTANDAO


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akihutubia katika kongamano la Kimataifa linalofadhiliwa na Serikali ya Denmark kupitia mpango wa kutumia michango ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET) lililofanyika Jijini Arusha.

Mratibu wa Mradi wa C4YET na Mhadhiri Mwandamizi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Nsubili Isaga akitoa maelezo ya awali katika kongamano la Kimataifa la kupitia mpango wa kutumia michango ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET) lililofanyika Jijini Arusha.

Washiriki wa kongamano la Kimataifa la kupitia mpango wa kutumia michango ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET) wakimsikiliza mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi, kongamono hilo la siku mbili limefanyika Jijini Arusha.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya ufunguzi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa William Mwegoha amesema tafiti mbalimbali zinazofanywa na wanataaluma wa chuo hicho zimelenga kuwainua vijana wa kitanzania kwa kuwapatia mitaji kupitia uchangiaji wa umati.

Profesa Mwegoha amesema hayo Januari 24, 2023 wakati wa uzinduzi wa kongamano la Kimataifa linalofadhiliwa na Serikali ya Denmark kupitia mpango wa kutumia michango ya umati kwenye kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania (C4YET ) lililofanyika Jijini Arusha.

Amesema tafiti hizo zimelenga kuangalia mbinu mbalimbali, faida kwa mlengwa na faida kwa mchangiaji ili kuwainua vijana na wajasiriamali wadogo wadogo kupitia uchangiaji wa umati.

“Kwa chuo chetu Mzumbe ni utafiti wenye manufaa makubwa kwasababu unachangia sana kwenye dhana ya Serikali ya kuhakikisha wajasiriamali wadogo wanawezeshwa mitaji” amesema Prof. Mwegoha.

Amesema kupitia kongamano hilo linalowakutanisha watalaamu kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo cha Copenhagen kutoka Denmark, watafiti watabadilishana matokeo ya utafiti na kupata njia sahihi yakutekeleza dhana ya uchangiaji wa umati.

Profesa Mwegoha amesema mradi huo ulianza mwaka 2019 na ni wa miaka mitano ambao umewanufaisha vijana wa maeneo yote ya mijini na vijijini.

Naye Mratibu wa mradi huo,Dkt. Nsubili Isaga kutoka skuli ya biashara Chuo Kikuu Mzumbe amesema mradi huo umewainua wajasiriamali kutokana na kubuni nyenzo walizotumia za uandishi wa andiko lililowavutia wafadhili kwaajili ya wanataaluma kusaidia tafiti na hatimaye chuo hicho kushirikisha SIDO kwaajili ya kuwakwamua wajasiriamali vijana kwenye mikoa mitano ambayo ni Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro na Mbeya.

Ameongeza kuwa jumla ya wajasiriamali 187 walipewa mafunzo hayo ambapo wajasiriamali 100 kati yao waliweza kupata mikopo yenye riba ya asilimia 5 tu inayowawezesha wao kurejesha mikopo yao kwa wakati na baadae vijana wengine watafikiwa zaidi ili wajiunge na majukwaa ya biashara mitandaoni

Previous articleMAB YAFANYA ZIARA KATIKA VIWANDA VYA DAWA NCHINI
Next articleAMEND TANZANIA- UBALOZI WA USWIS WATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here