Na: mwandishi wetu
Timu ya Mpira wa Kikapu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imerejea leo Ikitokea nchini Ujerumani ilipokuwa inashiriki Mashindano ya Majeshi ya Dunia na kufanikiwa kushika nafasi ya Nne Kati ya Nchi 22 zilizoshiriki Mashindano hayo.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Nchini Kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere, Kapteni Mohamed Kasui Mkuu Wa Msafara na timu meneja wa jeshi Amesema anashukuru kwa matokeo chanya waliyoyapata katika Mashindano hayo ya Three On Three World Championship na wanaahidi kuendelea kufanya vizuri Kwenye Mashindano mengine.
Kwa Upande wake Shendu Mwangala Mwenyekiti wa chama cha kikapu Dar es salaam, Amesema Ushindi huo Umeweza kulitangaza Jeshi na Taifa kwa ujumla kupitia mchezo wa kikapu kwani sio jambo dogo kwa mara ya kwanza kuweza kufanya vizuri.
Timu hiyo iliondoka Nchini Tanzania Julai,03,2022 Kuelekea Ujerumani katika mashindano Ya kidunia Ya Three On Three World Championship iliyoshirikisha timu kutoka mataifa mbalimbali Ikiwemo Marekani,Ufaransa,Saudi Arabia,Moroco.
Mwisho