Hayo yamesemwa Januari 04, 2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati akizindua Maktaba iliyojengwa na Bi. Jennifer Dickson Ugweno wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo Prof. Mkenda amesisitiza kuwa wadau Binafsi wanakaribishwa kuwekeza katika kujenga Maktaba maeneo mbalimbali nchini na kuwashukuru wadau waliojitoa kushiriki kujenga Maktaba hiyo ya Ugweno.
“Nichukue fursa hii kuwataka Wazazi wengine kuiga mfano wa Wazazi wa Jennifer kuanzisha Maktaba hii. Pia ninawasihi watoto wengine kuiga mfano huu wa kurudisha kwa jamii ili Taifa liendelee kupiga hatua kupitia Vijana wetu” alibainisha Waziri Mkenda.
Nae Mwanzilishi wa Maktaba Bi. Jennifer amesema ameanzisha Maktaba hiyo ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu kuhakikisha upatikanaji wa huduma hiyo katika eneo alilotoka.
“Maktaba hii pia ni mchango wangu na wa wale walioniunga mkono, katika kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuboresha sekta ya elimu nchini” alisema Jennifer.
Aisha amewashukuru Wanajumuiya wa Msangeni kwa michango yao pamoja na wafadhili mbalimbali ikiwemo Bayport Tanzania, Barrick Gold Mine Tanzania, Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT-MD).
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Bonaventure Rutinwa, amesema kuwa maktaba hiyo ni miundombinu ya kielimu inayomwezesha mtu wakiwemo watoto wadogo kupata elimu ya ziada kupitia usomaji wa vitabu.