Home BUSINESS UBUNIFU MAKINI WAIPA STAMICO USHINDI WA JUMLA

UBUNIFU MAKINI WAIPA STAMICO USHINDI WA JUMLA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse baada ya shirika hilo kuibuka mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner – Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimuangalia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse mara baada ya kumkabidhi tuzo ya ushindi kwa kwa shirika hilo baada ya kuibuka mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner – Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na mabalozi wa STAMICO baada ya kabidhi tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse baada ya shirika hilo kuibuka mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner – Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022 kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse akihojiwa na waandishi wa habari katika banda la STAMICO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse , Afisa Habari wa STAMICO Bibiana Ndumbaro na mabalozi wa STAMICO wakielekea kwenye banda lao mara baada ya kupokea tuzo hiyo.

Mabalozi wakiwa na tuzo huku wakiwa wameshika mkaa mbadala.

Na: Mwandishi wetu, DAR

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa jumla kwenye kipengele.a cha ubunifu makini (Overall Winner – Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.

Tuzo hiyo ya STAMICO imetolewa tarehe 13 Julai 2022 na Mgeni  rasmi Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kufunga maonyesho hayo.

Akipokea tuzo hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alisema, tunajivunia kupata tuzo hii ya jumla kutokana na ubunifu makini wa bidhaa bora ya mkaa mbadala wa kupikia (Rafiki Briquettes) unaotokana na Makaa ya Mawe. Mkaa huu ni njia madhubuti ya kuepusha ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya nishati.

Mkaa wa Rafiki Briquettes unaozalishwa na STAMICO ni Rafiki kwa mazingira, Rafiki kwa matumizi na Rafiki kwa bei. 
Pamoja na tuzo ya ubunifu, STAMICO vilevile walipewa cheti cha ubora wa mpangilio wa bidhaa (Certificate of high display standard).
Huu ni ushindi mara pili mfululizo kwa kipindi cha  miaka miwili, mwaka jana 2021 kwenye maonesho ya 45 ya Sabasaba STAMICO iliibuka mshidi wa kwanza wa jumla.

Tukio hili limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo, pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa.
Previous articleNIC YAUPIGA MWINGI MAONESHO YA SABASABA, YAPATA USHINDI WA KWANZA WATOA HUDUMA BORA ZA BIMA
Next articleSHAKA ATEMBELA VYOMBO VYA HABARI KISIWANI UNGUJA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here