Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama mahala pa kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akitoa mada katika kikao kazi kati ya Taasisi hiyo na Wahariri wa Habari kilichofanyika leo Disemba 7,2023 Jijini Dar es Salaam Chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Taasisi hiyo, Bi. Jane Mihanji akizungumza alipokuwa akitoa neno kwaa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deodaus Balile katika kikao kazi hicho.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Sabatho Kosuri akizungumza alipokuwa akitoa neno la ukaribisho mapema katika kikao hicho kilichofanyika leo Disemba 7.2023 Jijini Dar es Salaam.
Na: Mwandishi wetu
Wakala Mahali paKazi (OSHA) imesema kuwa kwa kushirikiana na wadau wanaanda mpango wa kutoa elimu juu ya athari za zinazotokana na matumizi ya simu kwenye vituo vya mafuta ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha na kuhepusha madhara yanayoweza kupatkkana.
Hayo yamebainishwa leo Disemba 7 Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda katika mkutano wake uliohusisha Wahariri na Waandishi wa Habari ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina wenye lengo la kueleza majukumu mbalimbali yanayofanya na Taasisi hiyo.
“Kushirikiana na wadau kutengeneza mpango wa kutambua matumizi ya simu kwenye vituo vya mafuta si salama kwa kutengeneza vibonzo kwaajili elimu zaidi watu waelewe si salama, kazi yetu kubwa OSHA ni kuzuia na kutoa elimu, “amesema Mwenda.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya jitihada za kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakuja kuwekeza nchini ikiwemo kuhimiza uboreshaji wa mazingira ya Biashara na uwekezaji na hili ni pamoja na maelekezo mbalimbali katika hotuba zake
Amesema kuwa wao kama OSHA wamefanya mapitio ya mlolongo wa shughuli zao “Business Process Review” na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika utoaji wa huduma zao.
“Baada yakufanya mapitio tukakuta kuna maeneo yanahitaji maboresho ambapo miongoni mwa maeneo yaliyoonekana kuwa na uhitaji wa maboresho ilikuwa kupunguza na kuondoa baadhi ya ada za huduma ambazo zisinge athiri usimamizi na utoaji wa huduma za usalama wa afya mahali pa kazi nchini,” amesema.
Amesema ada zilizofutwa ama kupunguzwa na OSHA zimeleta unafuu ambao unachochea ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini ikiwemo Kuongeza ajira kwa watanzania.
Ameeleza kuwa kiasi cha ada zilizopunguzwa zinakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 35 ambapo fedha hizo zitatumika katika kuhimarisha mifumo ya kulinda wafanyakazi waweze kuzalisha kwa tija.
Amesema mafanikio ya Wakala katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 kuhimarika kwa shuhuli za usimamizi mahala pa kazi nchini ambapo wakala umefanikiwa kuongea idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4336 hadi 30306 ongezeko hilo sawa na asilimia 599.
Aidha amesema idadi ya ukaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi 776,968 sawa na asilimia 646 kaguzi hizo zilizohusisha ukaguzi wa jumla.
Amesema Taasisi ya OSHA imefanikiwa kusimika mfumo wa TEHAMA wa usimamizi wa taarifa za kaguzi nchini ambapo kupitia mfumo huo huduma ya utoaji wa taarifa za ukaguzi ajali na mfumo unafanyika kwa njia ya kieletroniki.
Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili, Mwenda, amesema kuwa moja wapo ni baadhi ya waajiri kutotekeleza ipasavyo sheria namba 5 ya usalama na afya mahala pa kazi wanayosimamia ikiwemo kuto taarifa za ajali zinazotokea maeneo ya kazi.
Amesema, katiba ya nchi inasema kila binadamu ana haki ya kuishi inatambua hilo, na kwamba wana program ya kila kuhakikisha wanafika kwenye maendeleo yote kutoa elimu.
Mwisho.