Home LOCAL MAJALIWA AZINDUA MRADI WA REA WILAYANI MBOZI

MAJALIWA AZINDUA MRADI WA REA WILAYANI MBOZI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Songwe, Leo Novemba 24, 2023, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mradi wa usambazaji umeme vijijini na vitongojini, katika kijiji cha Ivugula kata ya Mahenje Wilaya ya Mbozi.

Mradi huo unaotekelezwa na wakala wa Umeme vijijini REA kwa thamani ya Shilingi Bilioni 5, unatarajiwa kusambaza umeme katika vitongoji 171 vya wilaya ya Mbozi, Ileje, Momba na Songwe.