Home LOCAL DKT.MAGEMBE ATAKA MAABARA BUBU KUFUNGIWA

DKT.MAGEMBE ATAKA MAABARA BUBU KUFUNGIWA

 

 

Na: Angela Msimbira TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshugulikia Afya Dkt. Grace Magembe amewaagiza waratibu wa huduma za maabara wa mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanazifungia maabara bubu zinazoendeshwa kinyume na utaratibu katika maeneo yao

Akifunga Kikao kazi cha waratibu wa Huduma za Maabara wa Mikoa na Halmashauri leo Jijini Dodoma Dkt Magembe amesema kuwa maabara bubu kwa sasa hazitakiwi kuwepo kwa kuwa kwa sasa Serikali imejipanga kuhakikisha inatoa huduma bora za afya kwa jamii

Amesema inashangaza kuona kuna viomgozi mbalimbali katika ngazi ya Kata, Halmashauri na Mkoa lakini bado kunakuwa na maabara bubu, timizeni majukumu yenu kwa kuhakikisha maabara hizo zinafungiwa kwa kuwa zinachafua taaluma ya maabara nchini.

Amewataka kuhakikisha maabara zote nchini zinasajiliwa na kutambulika na Serikali na wafanye kazi wakiwa na wataalam wenye ujuzi,weledi na kutoa vipimo ambavyo vinasaidia kuwapa matibabu wananchi.

“Zoezi hili la kuzikagua Maabara Bubu ziendane sambamba na maabara za Watu binafsi, pamoja na maabara za Serikali, kwa kuwa maabara zote zinatakiwa kufanyakazi kwa kuzingatia vigezo na masharti ya kitaaluma” amesisitiza Dkt Magembe.

Kuhusu kero za Wananchi amewataka kuhakikisha wanashughulikia kero za wananchi kwa kuwasikiliza na kusimamia utoaji wa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini

Dkt. Magembe amewataka kuhakikisha wanasimamia utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuangalia umahiri wa watumishi wa maabara ili kujua taaluma zao na uwezo wao katika kutoa huduma hiyo kwa jamii, kwa kuwa serikali inahitaji kutoa huduma bora kwa kutoa vipimo sahihi.

Previous article“MSIWE WACHOYO WA UJUZI” – WAZIRI GWAJIMA
Next articleSERIKALI YATOA WITO KWA BENKI YA NMB KUONGEZA UBUNIFU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here