Home BUSINESS SERIKALI YATOA WITO KWA BENKI YA NMB KUONGEZA UBUNIFU

SERIKALI YATOA WITO KWA BENKI YA NMB KUONGEZA UBUNIFU

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna walipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka benki hiyo, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza katika kikao na ujumbe kutoka Benki ya NMB ofisini kwake jijini Dodoma ambapo aliiagiza benki hiyo kujitahidi kupunguza mikopo chechefu.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Benki ya NMB ofisini kwake jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (hayupo pichani) mafanikio ya benki hiyo, walipokutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma.

Ujumbe kutoka Benki ya NMB ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna (kulia) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (hayupo pichani) walipokutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma.

 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano-WFM-Dodoma)

 Na:Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imetoa wito kwa Benki ya NMB kubuni huduma ambazo zitakidhi mahitaji  ya wananchi kulingana na mabadiliko ya mazingira.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Benki hiyo ofisini kwake jijini Dodoma.

Alisema mazingira yamekuwa yakibadili na mahitaji ya wananchi nayo yanabadilika kulingana na mazingira hivyo ni vyema benki hiyo iongeze jitihada za kukabiliana na mambo hayo ili kuwafikia wananchi na kuendelea kufanya vizuri katika soko.

“Na sisi kama Serikali tunaahidi kuwa tutaendelea kufanya kazi na nyinyi kwa kuhakikisha tunaweka mazingira mazuri ya kuwezesha Sekta hii ya fedha kukua kwa ustawi “, alisema Bw. Tutuba.

Aliitaka Benki ya NMB kuongeza jitihada katika kupunguza mikopo chechefu ambayo ni changamoto ya muda mrefu ingawa amebainisha kuwa baadhi ya mikopo hiyo imekuwa ikisababishwa na benki zenyewe.

“Hili la mikopo chechefu inabidi muwe makini sana katika kutathmini utoaji wa mikopo kwa wateja unakuta mteja hana historia nzuri ya masuala ya kibenki halafu mnamkopesha mnadhani nini kitatokea…”, alihoji Bw. Tutuba.

Katibu Mkuu huyo pia aliiagiza Benki hiyo kuongeza jitihada za kupunguza riba za mikopo kwa wateja wao, changamoto ambayo imekuwa ni ya muda mrefu kwa taasisi za fedha nchini.

Aidha, aliwasihi kuhakikisha wanaikumbuka sekta ya elimu katika shughuli zao za kurudisha fadhila kwa jamii, hususani katika kipindi hiki ambacho Serikali ipo katika jitihada za kuhakikisha inajenga madarasa na madawati ili kuhakikisha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani wanasajiliwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna aliahidi kuyatendea kazi maagizo yote yaiyotolewa na Serikali na kubainisha kuwa benki hiyo iko tayari kushirikiana na Serikali wakati wote.

Alisema benki hiyo iko viruzi kwa sasa katika nyanja tofauti tofauti ikiwemo uwekezaji, uendeshaji, mikopo pamoja na amana ambapo kwa mwaka jana benki hiyo ilipata faida ya Sh. bilioni 206 baada ya kodi na kutoa gawio la Sh. bilioni 68.5 kwa wanahisa wote, huku Serikali ikipata gawio la Sh. bilioni 21.8.

Previous articleDKT.MAGEMBE ATAKA MAABARA BUBU KUFUNGIWA
Next articleRAIS MHE.DKT.MWINYI AZINDUA BOTI ZA WANANCHI WA VISIWA VYA KAKOONGWE NA KISIWAPANZA BANDARI YA MKOANI PEMBA LEO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here