Home LOCAL MAJALIWA ATOA MAAGIZO KWA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU (HESBL)

MAJALIWA ATOA MAAGIZO KWA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU (HESBL)

Na Mwandishi wetu

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (HESBL) kufanya marejeo ya viwango vya mikopo vinavyotolewa kwa wanafunzi wa rubani ili kutoa kipaumbele kwa wahitaji wa fani za masuala ya usafiri wa anga.

Pia ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) kuimarisha mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege nchini visiwe vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu ili nchi iendelee kuwa na sifa ya kuwa kati ya nchi zenye udhibiti wa anga.

Maagizo hayo ameyatoa leo Oktoba jijini Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003 kwa malengo mbalimbali ikiwa kidhibiti na kusimamia huduma za usafiri wa Anga nchini.

“TCAA imarisheni mifumo ya udhibiti wa matumizi mabaya ya viwanja vya ndege haviwi vichochoro vya kusafirishia bidhaa haramu ili nchi iendelee kuwa na sifa ya kuwa kati ya nchi zenye udhibiti wa anga ,” amesema .

Majaliwa ametaka Mamlaka hiyo kujifunza kutoka Kwa mataifa yaliyofanikiwa ili kuiongeza viwango vya utoaji wa huduma na kuwa wabunifu wa hali ya juu kwa kuwa na mikakati ya kuimarisha soko ili nchi isiachwe nyuma kimaendeleo.

Aidha amesema wadau usafiri wa anga nchini, kutekeleza majukumu yao Kwa kufuata Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamiwa masuala ya usafiri wa anga kitaifa kwa ajili ya kuhakikisha usalama na kipaumbele namba Moja katika usafiri wa anga.

Vilevile aliitaka TCAA kubuni na kuongeza vyanzo vipyw vya mapato ya ‘Aviation Training Fund ‘ ili kuongeza idadi ya marubani wanaopata ufadhili wa masomo.

“Watanzania endeleeenu kuviamini na kutumia vyuo vilivyopo nchini kwani vinatoa mafunzo ya utalaamu wa anga wa uhakika,”.

Amesema serikali imepanga kuimarisha sekta ya anga kwa kuwezesha ununuzi wa rada za kisasa nne za kuongoza ndege za kiraia ambazo zimefungwa katika viwanja vya ngege vya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.

“Hivi karibuni, viwanja vya ndege vya AAKIA Zanzibar na JNAI vilikaguliwa na kupata asilimia 86.7 hatua hiyo imeowezesha nchi yetu kushika nafasi ya nne badani Afrika ikitanguliwa na nchi ya Nigeria ,Kenya, Ivory Cost, huu ni ushindani tosha kwamba uwezo wa nchi yetu katika kidhibiti usalama wa anga unaendelea kuimarika,”amesema.

MBARAWA

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Mbarawa aliwapongeza TCAA Kwa kusimamia ukaguzi huo na kuiweza nchi kupata alama 86.7 katika viwanja vya Dar es Salaam na Zanzibar.

Amesema serikali imeboresha miundombinu mbalimbali ya viwanja vya ndege hivyo kutokana na maboresho hayo anaamino ukaguzi ujao nchi itafikia asilimia 90.

MKURUGENZI
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCCA, Hamza Johari, alisema kuwa Mamlaka hiyo inaendeshwa Kwa kutumia mapato ya ndani haitegemei ruzuku ya serikali.

“Kwa miaka mitano tumekusanya bilioni 319.9 na bilioni 24.5 tumechangia katika mambo mbalimbali ya kijamii,”amesema Johari

Alisema TCCA imefungua mikataba mbalimbali ya usafiri Kwa nchi 80 hivi karibuni wameingia mkataba na nchi ya Marekani hivyo kuviwezesha ndage ya Air Tanzania kwenda kwenye nchi hiyo.

“TCCA wataacha kusomesha marubani nje ya nchi na kusomesha kwenye Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT) Kwa mwaka tulikuwa tunapeleka marubani 10 nje ya nchi sasa tunasomesha marubani 30 nchini na fedha kubaki nchini,”amesema.

Previous articleTAMKO LA KAMATI YA SERA YA FEDHA YA BENKU KUU YA TANZANIA 
Next articleTCAA YATOA UFAFANUZI KUHUSU KIBALI CHA NDEGE YA CHADEMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here