Leo Septemba 19,2021 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Rosemary Senyamule ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa ushiriki Bora katika Maonesho ya Nne ya Teknolojia ya Madini pamoja utumiaji wa tekinolojia katika uchimbaji wa madini.
Katika ziara hiyo ndani ya viwanja vya maonesho aliambatana na mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Nyang’hwale
Wakiwa katika mabanda hayo kwa pamoja wameipongeza Wizara kwa kushirikisha wananchi katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini.
Wakiwa katika Banda la GST wamefurahishwa na mpango wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa Madini unaotolewa na GST wenye lengo la kuleta tija katika uchukuaji wa sampuli wakilishi kwaajili ya uchunguzi na uchenjuaji wa madini.
Sambamba na hapo wameipongeza Tume ya Madini wa namna inavyoendelea kutoa huduma nzuri kwa wadau wa Sekta ya Madini pamoja na kuchangia katika kukuza pato la Taifa.
Kwa pamoja wamefurahishwa na namna STAMICO invyotoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa Madini hususani katika kuwashirikisha juu ya matumizi ya tekinolojia invyoweza kupunguza matumizi ya Zebaki.