Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania Kelvin Nyema (ambaye ni kiziwi wa kwanza kulia) akimuuliza swali Afisa Mauzo Mwandamizi wa NHC Daniel Kure huku mkalimani wao Naston Kagaruki akiwa tayari kutasfiri.
Odita Kandonga (wa kwanza kushoto) akiuliza swali huku mkalimani wao akimsikiliza kwa makini ili aweze kumweleza Daniel Kure nini ambacho anauliza.
“Siku moja tulikwenda EWURA kikazi, tukavutiwa na jengo lao na kuwapongeza kwa kuwa na jengo zuri, ndipo walipotuambia kuwa jengo lao limejengwa na NHC tukashangaa sana” Amesema Nyema.
Nyema ameipongeza NHC kwa utekelezaji wa miradi yake na kuishukuru sana kwani wao ni moja kati ya vijana waliobahatika kupewa mashine za hydraform zilizokuwa zikitolewa na NHC kwa makundi ya vijana.
Kwa upande wake mkalimani waliyeambatana naye Naston Kagaruki ambaye ndiye aliyekuwa akiwaeleza yale yanayosemwa na Afisa mauzo mwandamizi wa NHC Daniel Kure na yeye kueleza yale wanayoyasema viziwi hao, amesema kuwa vijana hao walipoliona banda la NHC walimshawishi waingie wana jambo la kusema.
Viziwi hao wanashiriki katika maonesho haya kutoka kundi la wachimbaji wadogo wa madini wanaofanyakazi katika mgodi uliopo eneo la Nyakafulu Wilaya ya Masumbwe Mkoa wa Geita.
Maonesho ya nne ya Teknolojia ya Uwekezaji Sekta ya Madini yanazijumuisha taasisi mbalimbali, makampuni na mabenki yanaendelea katika viwanja vya Bombambili – EPZ Mkoani Geita, yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Sekta ya Masini kwa Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu