Afisa Mfawidhi wa TASAC Rashid Katoka akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini jini Geita.
Katibu Tawala Wilaya ya Geita Dime akitia Saini kwenye Kitabu cha wageni mara baada ya kumaliza Ziara ya kutembelea kwenye Banda la TASAC.
Ofisa Mfawidhi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Geita Rashid Katonga amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao Shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu namna ambavyo shirika linavyotekeleza majukumu yake kwa mujubu wa sheria.
Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea jini Geita.
Amesema kuwa licha ya Majukumu makubwa waliyokuwa nayo pia limeendelea kutoa Elimu kwa wananchi namna shirikika lao linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
Ameongeza kuwa wapo kwenye maonesho hayo ili kuendelea kutoa elimu kwa umma na wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo, nakwamba kwa uwepo wao kwenye maonesho hayo wananchi wanapata fursa ya kujifunza shughili mbalimbali za Shirika hilo.
Maonesho hayo ya Teknolojia ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ni maonesho ya Nne kufanyika Mkoani Geita yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza Teknolojia za kisasa katika sekta hiyo pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo TASAC.