Home LOCAL MBUNGE BONAH: SERIKALI KUJENGA SHULE YA MSINGI MNYAMANI

MBUNGE BONAH: SERIKALI KUJENGA SHULE YA MSINGI MNYAMANI

NA: HERI SHAABAN, (ILALA YETU).

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amesema Serikali inatarajia kujenga shule ya Msingi Buguruni Mnyamani Wilaya ya Ilala .

Mbunge Bonah alisema hayo katika ziara yake ya Maendeleo Maendeleo pamoja na kutatua kero katika Kata ya Mnyamani,Bonyokwa na Kimanga .

“Serikali imezamilia kujenga shule ya Msingi eneo la Mnyamani Wilaya Ilala ili Wanafunzi wasiende kusoma shule za mbali itajengwa kupitia pesa za Serikali za mgao wa tozo” aliasema Bonah.

Bonah alisema Kata hiyo ya Mnyamani ilikuwa ina changanoto ya eneo la shule kwa sasa limepatikana eneo hilo la soko na baadhi ya Wananchi walio jirani ya eneo hilo wamekubali kulipwa fidia ili waweze kufanikisha ujenzi huo wa shule ya Msingi ambapo ifikapo January watoto wetu wasome.

Alisema Kata ya Mnyamani ni moja ya eneo lililokosa shule ya Msingi kwa sasa wananchi wamepata eneo hilo na wananchi wamekubali kulipwa fidia kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo hivyo mchakato wake wakati wowote unaannza.

“Taifa lolote ili liwe na Maendeleo lazima wananchi wake wapatiwe Elimu hivyo akuna budi Wananchi wangu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta ya Elimu bila malipo watoto wetu waweze kusoma ” alisema.

Aidha alisema juhudi hizo ni sehemu sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika kuwatumikia wananchi wake.

Katika Kata ya Bonyokwa  Mbunge akiongozana na Diwani wa kata hiyo  Tumike Malilo amekagua barabara inayopita Kituo cha Afya cha Harmony Memorial Polyclinic  ambapo alielezwa changamoto anazozipata mwekezaji wa kituo hicho cha Afya upande wa Miundombinu Mbunge ameahidi kuitafutia ufumbuzi changamoto ya barabara hiyo huku akimtaka Mhandisi wa Jiji la Dar es Salam John Magori   Kumfikishia taarifa Mkurugenzi wa jiji ili waweze kuchukua hatua za haraka za kutengeneza barabara hiyo.

Mhandisi Chacha Magori aliomba Diwani wa Bonyokwa Tumike Malilo kuitisha kikao cha Maendeleo na Wananchi kwa ajili ya ajenda ya Barabara hiyo ambayo wadau waanataka kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu.

Kata ya Kimanga mbunge Bonah  Wataalam   walikagua maendeleo ya mradi wa DMDP Phase 1 wa mfereji unaoanzia Maeneo ya Kwa Swai Tembo Mgwaza na kumtaka Mkandarasi kutekeleza mradi huo kwa haraka kwa kuzingatia uhitaji wa Wakazi hawa kwani wengine wameacha nyumba zao kwa sababu ya Mafuriko.

Mwisho

Previous articleYANGA YAAHIDI KUICHAPA KAGERA LEO
Next articleRC MAKALLA: ATANGAZA DAR SUNSET CARNIVAL COCO BEACH.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here