Kasulu, KIGOMA.
Maofisa wa Wakala ya Usajili wa biashara na leseni (BRELA) wamewapatia elimu ya namna ya kurasimisha biashara na umuhimu wa usajili wa nembo za biashara na kupata Leseni kwa wajasiliamali wadogo wanaoshiriki katika maonesho ya tatu ya SIDO Kitaifa yanayofanyika Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Wakitoa mada kwa wajasiliamali hao, Afisa Leseni wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Gabriel Gilangay ametoa mada juu ya umuhimu wa kusajili Jina la Biashara na Kampuni kwa wajasiliamali wanaoshiriki katika maonesho ya tatu ya SIDO kitaifa yanayofanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Akifafanua juu ya muhimu na faida za kusajili Bw. Gilangay amesema kuwa biashara zao zitapata kulindwa kisheria, utaweza kutambulika na Serikali kwakuwa utakuwa upo katika kanzidata, pia ukisajili biashara yako utaweza kupata mikopo ya biashara katika mabenki, pia utaweza kupata tenda zinazotangazwa ili kuweza kufanya biashara na makampuni na taasisi za Serikali na kuongeza kuwa ikiwa watafanya sajili za biashara na kampuni zao.
Naye Bw.Athuman Makuka kutoka katika idara ya Miliki Bunifu (BRELA), ametoa ufafanuzi juu ya sajili ya Alama ya Biashara na Vumbuzi ameeleza kuwa, ili uweze kupata usajili wa uvumbuzi ni lazima kitu hicho kiwe kitu kipya dunia nzima sio kwa hapa Tanzaniatu, na kwamba kiweze kushikika na pia uvumbuzi huo uweze kutatua changamoto katika jamii. Uvumbuzi huo baada ya kusajiliwa na BRELA utalindwa kwa muda wa miaka ishirini na baada ya hapo itakuwa ni mali ya umma.
Akizungumzia juu Alama za huduma na biashara kwa maana ya nembo ambayo inaweza kuwa Jina, Alama ama umbo ni lazima iwe ni ya kipekee, ili uweze kupata usajili , BRELA inaangalia upekee wa kitu ambacho utawasilisha kwa ajili ya kupata usajili. Baada ya kuwasilisha kuomba usajili wa nembo ni lazima iangaliwe kwamba isiwe inafanana na nyingine ambayo imekwisha sajiliwa hapa kwetu Tanzania.
Faida ya usajili wa alama ya biashara na huduma ama nembo ni kwambwa unapata faida ya kulindwa kisherika, pia baada ya kusajili nembo utakaa kwa muda wa miaka saba ndipo atalipia tena. Ada ya usajili wa nembo ni shilingi Laki moja na Elfu Thelasini tu (130,000/= ambayo huilipi yote mara moja,
Wakati huohuo Afisa Leseni Bw. Rajab Chambega ameeleza juu ya upatikanaji wa aina mbili za leseni yaani leseni ya kiwanda na leseni ya biashara. Pia ametolea maelezo ya makundi mawili ya leseni ambazo zinatolewa na BRELA chini ya Wizara ya viwanda na biashara ambazo ni Leseni ya biashara kundi A na aina ya pili ni Leseni ya biashara kundi B ambazo hutolewa na Halmashauri chini ya TAMISENI
Pia ameelezea juu ya viambata vinavyohitajika katika uombaji wa Leseni kwa kutumia jina la Biashara na Makampuni pamoja na Adaza za usajili wa cheti / leseni ya kiwanda ni pamoja na (NIDA, ama Cheti cha Kuzaliwa ama Paspot), pili uwe na Tin namba, pia uthibitisho wa eneo la biashara (mkataba wa pango) .