Home LOCAL UFARANSA KUFANYA MKUTANO MKUBWA KUJADILI MAHUSIANO MAPYA KATI YAKE NA AFRIKA

UFARANSA KUFANYA MKUTANO MKUBWA KUJADILI MAHUSIANO MAPYA KATI YAKE NA AFRIKA

 

DAR ES SALAAM.

NCHI ya Ufaransa imeaanda mkutano mkubwa unaotarajia kufanyika Oktoba 8 mwaka huu katika Mji wa Montpellier ambapo mkutano huo unakwenda kuwakutanisha wadau kutoka kila pembe ya Afrika kwa ajili ya kujadili na kujenga uhusiano mpya kati ya Ufaransa na Afrika.

Wakati wa Mkutano huo utazingatia “Madereva wa mabadiliko” na kwamba mamia ya watu kutoka Afrika wakiwemo Wasanii, watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati wa mazingira, watafiti, bingwa wa michezo, wajasiriamali wachanga, washawishi na waandishi wa habari.

Mkutano huo unakusudia kutoa changamoto na kufafanua upya misingi ya uhusiano kati ya Ufaransa na Afrika kwa kuwasikiliza vijana, kujibu maswali yao na kutoa jukwaa jipya la mazungumzo yaliyolenga siku zijazo.

Akizungumza zaidi mkutano huo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui ambaye anatarajia kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibu amesema katika mkutano huo kutakuwa na majadiliano yatakayowaleta pamoja kujadili mustakabali wa uhuasiano mwema kati ya nchi hiyo na Afrika.

“Wakati wa mkutano huo, Emmanuel Macron, Rais wa Jamhuri ya Ufaransa atakuwa na mjadala wa wazi na wawakilishi 10 wa vijana wa Kiafrika kuhusu kuusuka  upya kwa uhusiano wa Afrika na nchi ya Ufaransa. Na Mkutano huu utakuwa wazi  ili kutoa uwanja mpana wa majadiliano zaidi kufanikisha malengo ya mkutano,”amesema.

Katika mkutano huo Tanzania itawakilishwa vyema na watu 16 wakiwemo  wajasiriamali, watetezi wa haki za binadamu, viongozi kutoka Asasi za kiraia, wasanii.Miongoni mwa Watanzania hao ni Seven Mosha ambaye ni Mkurugenzi wa Label ya  Sony Afrika Mashariki (Masoko, Wasanii) na Mchoraji maarufu wa Vibonzo Meddy ambaye pia anafanya kazi RFI na Courrier International.

Balozi Hajlaoui amesema katika kuelekea mkutano huo Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umeamua kuandaa Mdahalo uliowakutanisha wadau wa sekta ya sanaa kujadili namna ya kukuza Ubunifu.

Akifafanua zaidi akiwa katika Kkituo cha Ufaransa cha Utamaduni  kinachoitwa Alliance Francaise de Dar es Salaam Balozi Hajlaoui amesema wameandaa matukio mawili kusaidia Ubalozi wa  Ufaransa  kuchambua uhusiano kati ya Ufaransa na Tanzania na kutambua fursa za ushirikiano kwa siku zijazo.

“Kwanini Ubalozi wa Ufaransa upange hafla mbili za mapema kuandaa mkutano huo?, Mijadala hii miwili, wa kwanza usiku wa leo ililenga Jinsi watu wanavyoweza kupata fedha kupitia Mawazo? Na ya pili itafanyika  Septemba 23 Alliance Francais  kutakuwa na mkutano ambao utazingatia Ubunifu, kuanzisha, kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa”.

Hivyo amesema wakati wa Mkutano huo  wa Oktoba  8 mwaka huu mtu yeyote anaweza kuchangia katika mpango huo  wa ushirikiano ambao haujawahi kutokea ambao pia  utarushwa Live kupitia media ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na LinkedIn) na kwenye tovuti ya sommetafriquefrance.org.

Raia, wasomi na washawishi watahusika katika safu ya hafla za AfricaFranceRemix kuandaa Mkutano Mpya wa Afrika na Ufaransa.

Credit – Michuzi Blog.

 

Previous articleBRELA YATOA SOMO KWA WAJASIRIAMALI KURASIMISHA BIASHARA ZAO
Next articleMAGAZETI YA LEO J.MOSI OCTOBA 2-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here