Home LOCAL PROF. KITILA MKUMBO AWAUNGA MKONO WANANCHI MAVURUNZA UJENZI WA BARABARA

PROF. KITILA MKUMBO AWAUNGA MKONO WANANCHI MAVURUNZA UJENZI WA BARABARA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. @kitilam ameunga mkono juhudi za Wananchi wa Shina namba 7 mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara wilayani Ubungo kwa kuchangia mifuko 50 ya saruji ili kuendeleza ujenzi wa barabara ya zege.

Pamoja na mifuko hiyo ya saruji Prof. Kitila ameahidi kutoa kiasi cha Sh. Milioni 2.4 ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi huo wa barabara yenye urefu wa mita 1,200.

Akikabidhi saruji hiyo baada ya kukagua ujenzi wa barabara ambao umetekelezwa Kwa nguvu za Wananchi urefu wa mita 800 Waziri Prof. Kitila ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo amewapongeza wananchi hao kwa kujitolea kufanya maendeleo kwenye eneo lao.

“Siku zote tunahimiza wananchi washiriki kuleta maendeleo na ninyi mmetekeleza hilo, kwa upande wa Serikali itajenga kwa kiwango cha Lami barabara ya Kikwete Highway na tayari wametoa Sh. Bilioni moja kwaajili ya hatua za awali ” amesema Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

“Kwenye eneo lenu niliahidi Kikwete Highway ambayo ipo kwenye utekelezaji na barabara ya Suka-Golani ambayo imeingizwa kwenye mpango wa DMDP na ipo kwenye upembuzi yakinifu zikikamilika hizi tutakuwa tumepiga hatua “ amesema Prof. Kitila.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kimara Ismail Mvungi amesema changamoto kubwa ya Kata ya Kimara ni barabara za mitaani na kuwataka wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo kwenye maeneo yao naye atakuwa nao bega kwa bega.

“Kila siku nitakuwa nakuja hapa kushirikiana na ninyi mpaka tukamilishe mita zote 1,200 haya ndiyo maendeleo ambayo Serikali yangu inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) inataka” Ismail Mvungi Diwani Kata ya Kimara

Naye Mjumbe wa Shina namba 7 mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara Asha Mwakipesile amesema kufuatia changamoto ya miundombinu katika mtaa wao waliamua kuchangishana fedha za ujenzi kiasi cha Sh. Milioni 25 na kujenga mita 800 za barabara ya zege.

Amesema kabla ya ujenzi huo wanafunzi wamekuwa wakishindwa kwenda shule nyakati za mvua huku shughuli nyingine za maendeleo nazo zikilala.

Asha amemshukuru Mbunge wao ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo kwa kuwachangia mifuko 50 ya saruji na Shilingi milioni 2.4

Mwisho

Previous articleTANZANIA NA AFRIKA KUSINI ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA AFYA
Next articleWAFANYABIASHARA MAWEZI WANOLEWA MATUMIZI YA MIZANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here