Home LOCAL TANZANIA NA AFRIKA KUSINI ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA AFYA

TANZANIA NA AFRIKA KUSINI ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA AFYA

Johanesburg, Afrika ya Kusini

 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Afya baina ya nchi hizo mbili ili kuweza kuboresha zaidi huduma za afya na ushirikiano wa pamoja katika kubadilishana uzoefu na watalaam wa Afya.
 
Makubaliano hayo yamefanyika Septemba 1, 2023 kupitia Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya Afrika Kusini Mhe. Dkt. Mathume Joseph Phaahla Jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambapo Viongozi hao wamekubaliana kuwa na mpango wa utekelezaji na ufuatiliaji wa mkataba huo na kutoa taarifa kila mwaka.
 
“Tanzania na Afrika Kusini zimekuwa na ushirikiano wa muda katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya, kusainiwa kwa hati hii kutachangia  kuboresha ushirikiano katika sekta ya Afya ikiwemo kubadilishana wataalam wabobezi kwenye fani mbalimbali za afya, kuwezesha mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu na kubadilishana teknolojia, kuboresha upatikanaji wa dawa, chanjo na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko pamoja na dharura za Afya”Amesema Waziri Ummy na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaimarisha mfumo wa huduma za  rufaa kwa wagonjwa watakaohitaji matibabu nchini Afrika Kusini.
 
“Kusainiwa kwa hati hii moja ya maazimio ya Mkutano wa Pili wa mataifa mawili( Bi – National Commission – BNC)  baina ya  Tanzania na Afrika kusini ambapo  Azimio Na. 43 lilielekeza kwamba, Hati ya Makubaliano katika sekta ya Afya isainiwe  baada ya taratibu zote ambapo Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini walisisitiza umuhimu wa kutekeleza maafikiano yaliyofikiwa na kutoa mrejesho wa utekelezaji kwa wakati” amefafanua Mhe. Ummy.
 
Kwa upande wake Mhe.Dkt. Phaahla, Waziri wa Afya wa Afrika Kusini amepongeza hatua ya kusainiwa kwa hati ya makubaliano haya ambayo imefanyika katika kipindi ambacho nchi za  Dunia nzima na Bara la Afrika zikiwemo nchi za Afrika Kusini na Tanzania zinakabiliwa na majanga mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi inayopelekea milipuko ya magonjwa na ukosefu wa vyakula.
 
Utiaji saini wa makubaliano haya ni utaimarisha zaidi ushirikiano katika masuala yaliyoanzishwa kama vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa, wakala wa dawa, mifumo ya ununuzi wa pamoja wa dawa” ameeleza Mhe. Dkt. Phaahla.

  

Previous articleRAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA POSTA AFRIKA.
Next articlePROF. KITILA MKUMBO AWAUNGA MKONO WANANCHI MAVURUNZA UJENZI WA BARABARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here