Na: Stella kessy.
KIUNGO mkabaji Sadio Kanoute, jana ameunga na wenzake katika mazoezi baada ya kupona maumivu ya bega aliyopata katika mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Yanga Septemba 25 mwaka huu.
Kanoute ni raia ya Mali amekosa mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Biashara United pamoja na Dodoma Jiji kutokana na majeruhi.
Huku kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho yeye ataendelea kukaa nje kwa wiki moja zaidi akiendelea kuuguza jeraha la enka chini ya uangalizi wa daktari alilopata katika mchezo uliopita dhidi ya Dodoma jiji.
Baada ya mapunziko ya siku mbili na kikosi jana kimeanza mazoezi katika uwanja wa boko Veterans na wachezaji ambao hawajaitwa kwenye kikosi timu zao za taifa.
Wachezaji wa simba 16 wameitwa kwenye timu zao za taifa hivyo waliobaki wamechanganywa na timu ya vijana kufanya mazoezi ili walimu waendelee na program yao.