Home SPORTS SADIO KANOUTE AUNGANA NA WENZAKE MAZOEZINI

SADIO KANOUTE AUNGANA NA WENZAKE MAZOEZINI

Na: Stella kessy.

KIUNGO mkabaji Sadio Kanoute, jana ameunga na wenzake katika  mazoezi baada ya kupona maumivu ya bega aliyopata katika mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Yanga Septemba 25 mwaka huu.

Kanoute ni raia ya Mali amekosa mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Biashara United pamoja na Dodoma Jiji kutokana na majeruhi. 

Huku kiungo mshambuliaji Pape Ousmane  Sakho yeye ataendelea kukaa nje kwa wiki moja zaidi akiendelea kuuguza jeraha la enka chini ya uangalizi wa daktari alilopata katika mchezo uliopita dhidi ya Dodoma jiji.

Baada ya mapunziko ya siku mbili na kikosi jana kimeanza mazoezi katika uwanja wa boko Veterans na wachezaji ambao hawajaitwa kwenye kikosi timu zao za taifa.

Wachezaji wa simba 16 wameitwa kwenye timu zao za taifa hivyo waliobaki wamechanganywa na timu ya  vijana kufanya mazoezi ili walimu waendelee na program yao.

Previous articleGGML YASAINI MKATABA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KAGERA
Next articleKIKOSI CHA YANGA KUWEKA KAMBI ARUSHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here