Na. Josephine Majura, WF, Dar es Salaam
Serikali imewaalika wadau wa Sekta Binafsi kutoka Uingereza kuwekeza nchini ili kusaidia juhudi za Serikali kufikia malengo yake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey.
Mhe. Chande alisema Serikali imekamilisha utiaji saini na UK Export Finance kwenye Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na kuendeleza barabara ya Tunguu – Makunduchi -kilomita 28, Fumba – Kisauni-Mazizini -kilomita 13.2, na mkoani – Chake Chake and Pemba Airport kwa ukubwa wa kilomita 43.5
Katika kikao hicho Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Chande aliwakaribisha Wawekezaji mbalimbali kutoka Uingereza kuja kuwekeza katika sekta za uzalishaji, uongezaji thamani na utalii nchini Tanzania.
“Nakukaribisha wewe na wafanyabiashara na wawekezaji wa kiingereza kuleta mitaji yenu Tanzania ” alisema Chande.
Kwa upande wake Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey Humphrey, alisema watashirikiana na Serikali kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika na kuendekeza kuwekeza katika vipaumbele vya kibiashara vilivyopo nchini Tanzania.