Home LOCAL DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWIZI NCHINI TANZANIA

DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWIZI NCHINI TANZANIA

Na.WAMJW- DSM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambapo wamekubaliana kuimarisha mahusiano na mashirikiano kati ya Tanzania na Uswisi.

Dkt. Gwajima amemhakikishia Balozi huyo kuendelea kusaidiana na Serikali ya Uswisi na katika mazungumzo yao wote wawili wamekubaliana kufadhili uimarishaji mfuko wa afya ya pamoja (HBF), mifumo ya afya pamoja na huduma zote za mtandao katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Naye, Balozi Mhe. Didier Chassot amesema Uswisi iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya hususani katika swala zima la kuimarisha mifumo ya vituo vya afya na huduma za mtandao.

Viongozi hao wamekutaka na kufanya mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo za Wizara mkoani Dar es Salaam, ambapo kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe OR- TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Previous articleSERIKALI YA TANZANIA YAFANIKIWA KUTEKELEZA KAULI MBIU YA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU CHAKULA
Next articleMEYA KUMBILAMOTO AIPONGEZA BENKI YA BIASHARA TCB
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here