Timu ya Mitaa ya Jangwani Jijini Dar es Salaam, Yanga SC imefanikiwa kutingĂ kwenye hatua ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika, kwa kuitandika magoli 5-1 Timu ya Asas Djibouti katika Azam Complex Jijini Dar es Salaam.
Katika Mchezo huo, Timu ya Yanga walianza kupata bao la kwanza dakika ya 7 likifungwa na Max Mpia Nzengeli kwa kichwa akimalizia pasi ya Jesus Moloko.
Yanga SC waliendelea kucheza kwa nguvu na Kasi kubwa wakilisakama lango la Asas ambapo mnamo dakika ya 45 Mshambuliaji Hafiz Konkini alifunga goli la pili akimalizia Mpira wa Stephane Aziz Ki na kuwafanya vijana hao wa Jangwani kwenda mapumziko kifuta mbele kwa uongozi wa magoli 2.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku Timu zote zikishambuliana, huku Yanga SC wakendeleza wimbi la ushindi.
Mnamo dakika ya 85 ya mchezo huo, Asas Djibouti walipata bao kwa Mkwaju wa Penalti na Tito Mayor baada ya Kiungo Mkabaji Gift Mauya kucheza rafu ndani ya 18 na mwamuzi kuamua kuwa Penalti.
Max Mpia Nzengeli alirudi tena kwenye kamba mnamo dakika ya 90 + 1 akifunga bao la tano baada ya kumalizia Mpira wa Clement Mzize.
Kwa ushindi Yanga SC wameiondosha Asas Djibouti jumla ya mabao 7-1 baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa mabao 2-0 na sasa rasmi itaanza ugenini dhidi ya El Merreikh ya Sudan ambao wamechagua kutumia uwanja wa Huye uliopo nchini Rwanda.