Na: Stella Kessy.
TIMU ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imetwaa ubingwa wa Cosafa kwa kuichapa Malawi bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa huko Afrika ya Kusini.
Hata hivyo kikosi cha Twiga kimefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu ianze kualikwa na mwaka 2011 ilimaliza nafasi ya tatu.
Katika dakika za 64 Enekia Kasonga ambaye ameifanikisha Tanzania kuweza kutwaa ubingwa na bao hilo limedumu katika dakika zote 90.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa ngumu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho kwani mbali ya Twiga kushinda Malawi ilionekana kulisakama vyema lango lao lakini umakini ulisababisha wasipate nafasi ya kusawazisha.
Kwa upande wa mchezaji bora wa mchezo huo ilichukuliwa na Kapteni wa Twiga Amina Bilal ambaye pia alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.