Home SPORTS TWIGA STARS YABEBA UBINGWA WA COSAFA

TWIGA STARS YABEBA UBINGWA WA COSAFA


Na: Stella Kessy.

TIMU ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imetwaa  ubingwa wa Cosafa kwa kuichapa  Malawi bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa huko  Afrika ya Kusini.

Hata hivyo kikosi cha Twiga kimefanikiwa  kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu ianze kualikwa na mwaka  2011 ilimaliza nafasi ya tatu.

Katika dakika za 64  Enekia Kasonga ambaye ameifanikisha Tanzania kuweza kutwaa ubingwa na bao hilo limedumu katika dakika zote 90.Katika mchezo huo ambao ulikuwa ngumu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho kwani mbali ya Twiga kushinda Malawi ilionekana kulisakama vyema lango lao lakini umakini ulisababisha wasipate nafasi ya kusawazisha.

Kwa upande wa  mchezaji bora wa mchezo huo ilichukuliwa na Kapteni wa Twiga Amina Bilal ambaye pia alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.

Previous articleTANZANITE YAICHAPA ERITREA
Next articleDKT. ABBASI: SERIKALI YA RAIS SAMIA INA JAMBO NA MICHEZO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here