Home LOCAL CHUO KIKUU MZUMBE KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA MAONESHO YA TCU JIJINI DAR

CHUO KIKUU MZUMBE KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA MAONESHO YA TCU JIJINI DAR

Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Bi. Rose Joseph, (kulia) akizungumza na Mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ni mmiliki wa Fullshangwe Blog John Bukuku  9wa kwanza kulia) katika Banda la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu Julai 19,2022 katika viwanza vya mnazi mmoja Jijini dar es Salaam.

Chuo Kikuu Mzumbe ni moja kati ya Taasisi za Elimu ya Juu nchini zilizoshiriki katika maonesho hayo ambapopamoja na mambo mengine Mzumbe wanafanya udahili wa Papokwa hapo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliohitimu kidato cha sita na wale waliomaliza masomo ya Diploma.

Aidha Mzumbe pia kabla ya kufanya udahili wanatoa ushauri kwa wanaotaka kujiunga na chuo hicho kuhusu fani wanazoweza kusomea kulingana na ufaulu wao wa kidato cha sita na ngazi ya Diploma ili kufanya uchaguzi sahihi wa masomo watakayosoma.

Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Bi. Rose Joseph, akiendelea na shughuli mbalimbali za udahili kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na kozi zinazotolewa na Chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2022/23.

Afisa Udahili wa Chuo Kikuu Mzumbe dambaye pia ni Mratibu wa Kituo cha Msaada wa sheria wa chuo hicho Bernadetha Iteba akifurahia jambo alipokuwa akiendelea na zoezi la Udahili kwenye Banda la Chuo hicho kwenye Maoesho ya TCU Jijini Dar es Salaam.

Maofisa wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiendelea na kazi ya Udahili kwenye banda lao katika maonesho hayo. PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO
Previous articleMWEKEZAJI KIWANDA CHA JIELONG AFUNGUKA CHANGAMOTO YA UHABA WA MALIGHAFI..ASHAURI UZALISHAJI MAZAO YA MAFUTA
Next articleKUTOKA MAGAZETINI ASUBUHI YA LEO JUMATANO JULAI 20-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here