Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuwahudumia watanzania kwa kutoa huduma Bora za Bima alipotembelea Banda la Shirika hilo katika Maonesho ya Nanenane yaliyofunguliwa rasmi leo Agosti 1,2023 katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Dkt. Mpango amelipongeza Shirika la Bima la NIC kwa kubuni bima ya Kilimo kwa ajili ya wakulima kwa sababu wakulima walikuwa kama wamesahaulika, hivyo ujio wa bima hiyo ni ukombozi kwa wakulima wa hapa nchini na kwamba itasaidia kuwa na uhakika wa shughuli zao za kilimo.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amesema Wizara ya Kilimo ilianza programu ya bima ya Kilimo kwa kuanza na shirika la bima la NIC, baada ya bima hiyo kuonesha mafanikio sasa makampuni mengine ya bima pia yameanza kutoa huduma hiyo kwa wakulima.
Mpaka sasa zaidi ya wakulima 500 wamejiunga na Bima hiyo ambapo pia wakulima walipo katika Vyama vya Ushirika zaidi ya 200 katika mikoa mbalimbali hapa nchini wamenufaika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipata akipokelewa na Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Justine Seni, (wa pili kulia), na Afisa Habari Mwandamizi wa Shirika hilo, Ephrancia Mawalla (kulia), mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili katika Banda la Shirika hilo kujionea shughuli wanazofanya katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.Â
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Justine Seni (wa tatu kulia), mara baada ya Makamu wa rais kuwasili katika Banda la Taasisi hiyo kujionea shughuli wananzofanya katika maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati alipotembelea banda la NIC katika maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023, wa pili kutoka kulia ni Justine Seni Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Justine Seni (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wenzake wa Shirika hilo, katika Banda lao.
Muonekano wa Banda la NIC
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)