Free Porn
xbporn
Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AZINDUA HUDUMA ZA MRI HOSPITALI YA KANDA MBEYA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA HUDUMA ZA MRI HOSPITALI YA KANDA MBEYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Huduma ya Mashine ya MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 01 Agosti 2023. (kutoka kulia ni Spik awa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera,Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji.

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi pamoja na wahudumu mbalimbali wa afya mara baada ya kuzindua Huduma za Mashine ya MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 01 Agosti 2023.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasikiliza vijana wabunifu waliotengeneza gari maalum za kupokea na kusafirisha wagonjwa katika maeneo ya hospitali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma za Mashine ya MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 01 Agosti 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali ya awamu ya sita ina dhamira ya dhati kuhakikisha huduma bora za afya zinasogezwa Jirani na wananchi.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za mashine ya MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya iliogharimu shilingi bilioni 3. Amesema kusogezwa kwa huduma bora kama uwepo wa MRI katika hospitali hiyo ni lengo la kuwapunguzia wananchi gharama na adha za kufuata huduma hizo maeneo ya mbali.

Makamu wa Rais ameupongeza uongozi na wahudumu katika hospitali hiyo kwa kuendelea kujitoa katika kuwahumia wananchi na ubunifu walioufanya katika kutafuta vifaa mbalimbali ikiwemo vya kusafirisha wagonjwa ndani ya hospitali.

Aidha ametoa wito kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kuzingatia utunzaji wa MRI hiyo ikiwemo kuzingatia muda maalumu wa matengenezo uliopangwa ili itoe huduma kwa muda mrefu.

Pia ameagiza Wizara ya Afya kukamilisha utaratibu unaopaswa ili kuifanya Hospitali hiyo kuwa taasisi na kujiendesha kiufanisi zaidi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema wabunifu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wako katika hatua za mwisho kutengeneza kifaa maalum kinachowekwa mkononi kwa mgonjwa kitakachoweza kutuma ripoti kwa daktari muda wote hali ya hali ya mgonjwa inavyobadilika  hata akiwa mbali na hospitali. 

Amewapongeza wabunifu katika hospitali hiyo kwa kutumia rasilimali ziliozopo kubuni masuluhisho mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora hospitalini.

Previous articleDKT MPANGO AIPONGEZA NIC KUANZISHA BIMA YA KILIMO
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO AGOSTI 2-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea MAKAMU WA RAIS AZINDUA HUDUMA ZA MRI HOSPITALI YA KANDA MBEYA