Hivi karibuni kuimeibuka wimbi la vitendo vya matumizi mabaya ya noti katika shughuli mbalimbali za kijamii hususan kwenye sherehe za harusi ambapo watu wamekuwa na tabia ya kutunza wahusika wa matukio kwa kuwarushia noti zinazoanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa, kuziviringisha katika maumbo mbalimbali na kutumia kama mapambo, kuweka kwenye mwili wa mtu ulio loa jasho na matukio yote yanayofanana na hayo.
Matendo haya yanatweza fedha ya Tanzania ambayo ni moja ya tunu za taifa letu.Vitendo hivyo vinaendelea kutokea licha ya Benki Kuu ya Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa nyakati tofauti kuvikemea.
Hivyo basi, Benki Kuu ya Tanzania inatoa onyo kwa wananchi ambao bado wanakaidi onyo hili ambalo limetolewa mara kadhaa kuhusu namna sahihi ya kutunza noti za Tanzania zinazokuwa mikononi mwao kwa kuzitumia kinyume na maadili pamoja na matakwa ya kisheria.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania itaanza kuchukua hatua dhidi ya wale wote watakaohusika na vitendo vya matumizi mabaya ya noti za Tanzania kwa njia yoyote ile ikiwamo kuweka pesa sakafuni au sehemu yoyote ambayo siyo nadhifu. Vitendo hivyo vinachangia kutweza fedha zetu na kusababisha uchakavu hivyo kuiongezea Serikali gharama kubwa za kuchapisha fedha zingine.
Aidha, Benki Kuu inawashauri washiriki katika matukio yote ambayo yanahusisha matumizi ya fedha kuandaa vyombo maalum vya kuweka fedha hizo badala ya kufanya vitendo ambavyo havikubaliki.
Wananchi wote mnahamasishwa kutoa taarifa mara moja kwa Benki Kuu au Vyombo vya Usalama pale mnapobaini matumizi yasiyo sahihi ya fedha zetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Tukitunza fedha zetu tunachangia kuzifanya zitumike kwa muda mrefu na hivyo kuipunguzia Serikali