Home BUSINESS BENKI KUU KUANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA NOTI

BENKI KUU KUANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA NOTI

Hivi karibuni kuimeibuka wimbi la vitendo vya matumizi mabaya ya noti katika shughuli mbalimbali  za kijamii hususan kwenye sherehe za harusi ambapo watu wamekuwa na tabia ya kutunza wahusika  wa matukio kwa kuwarushia noti zinazoanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa, kuziviringisha katika maumbo mbalimbali na kutumia kama mapambo, kuweka kwenye mwili wa  mtu ulio loa jasho na matukio yote yanayofanana na hayo.  

Matendo haya yanatweza fedha ya Tanzania ambayo ni moja ya tunu za taifa letu.Vitendo hivyo  vinaendelea kutokea licha ya Benki Kuu ya Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa nyakati  tofauti kuvikemea. 

Hivyo basi, Benki Kuu ya Tanzania inatoa onyo kwa wananchi ambao bado wanakaidi onyo hili  ambalo limetolewa mara kadhaa kuhusu namna sahihi ya kutunza noti za Tanzania zinazokuwa  mikononi mwao kwa kuzitumia kinyume na maadili pamoja na matakwa ya kisheria. 

Kwa taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania itaanza kuchukua hatua dhidi ya wale wote watakaohusika  na vitendo vya matumizi mabaya ya noti za Tanzania kwa njia yoyote ile ikiwamo kuweka pesa  sakafuni au sehemu yoyote ambayo siyo nadhifu. Vitendo hivyo vinachangia kutweza fedha zetu na kusababisha uchakavu hivyo kuiongezea Serikali gharama kubwa za kuchapisha fedha zingine. 

Aidha, Benki Kuu inawashauri washiriki katika matukio yote ambayo yanahusisha matumizi ya fedha  kuandaa vyombo maalum vya kuweka fedha hizo badala ya kufanya vitendo ambavyo havikubaliki. 

Wananchi wote mnahamasishwa kutoa taarifa mara moja kwa Benki Kuu au Vyombo vya Usalama  pale mnapobaini matumizi yasiyo sahihi ya fedha zetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi  ya wahusika. 

Tukitunza fedha zetu tunachangia kuzifanya zitumike kwa muda mrefu na hivyo kuipunguzia  Serikali

Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI OCTOBA 28-2021
Next articleBENKI YA NBC YAJA NA KADI MPYA,MTEJA ANAWEZA KUFANYA MIAMALA HADI YA MILIONI 40 KWA MARA MOJA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here