Home BUSINESS TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI MWAKA WA MASOMO 2023-2024

TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI MWAKA WA MASOMO 2023-2024

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumzia na waandishi wa Habari katika Ofisi za Tume zilizopo Jijini Dar es Salaam, kuelezea kufunguliwa kwa Dirisha la Udahili kwa mwaka wa masomo 2023-2024.

(PICHA NA: FRANCIS DANDE)

DAR ES SALAAM.

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua Dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kuanzia leo Julai 15, 2023 kwa kuzingatia sifa na vigezo stahiki za waombaji zinazohitajika.

Akizungumzia na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa amesema Dirisha litakuwa wazi hadi Agosti 4, 2023 na kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU au tovuti za Vyuo mbalimbli vinavyotoa elimu ya Juu.

“Waombaji wote wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2023/2024 wanatakiwa kuwa na sifa stahiki za kidato cha sita, sifa stahiki za Stashahada na Cheti cha awali.

“Maombi ya udahili wa kujiunga na shahada ya kwanza utahusu waombaji waliohitimu kidato cha sita, wenye Stashahada (Ordinary Diploma), na wenye sifa stahili za cheti cha awali (Foundation Certificate) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)” amesema Prof. Kihampa.

Aidha ameongeza kuwa ili kufahamu sifa stahiki za kujiunga na Chuo Kikuu, waombaji wameelekezwa kusoma vigezo vilivyopo kwenye vitabu vya muongozo vya TCU huku pia wakitakiwa kutuma maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo wamevichagua na kwamba maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi yanayotolewa na vyuo vikuu husika.

Pia, ametoa tahadhari kwa waombaji wote wa shahada ya kwanza ikiwa watahitaji kupata ufafanuzi wa suala lolote juu ya udahili kuwasiliana moja kwa moja na vyuo husika ama TCU.

“Tunawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini” amesema Prof. Kihampa.

Katika hatua nyingine, Prof. Kihampa amewakaribisha wadau wote kushiriki maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, kuanzia Julai 17 hadi 22 mwaka huu ambapo vyuo 80 vinatarajiwa na kwamba wananchi hususani wanafunzi watapata fursa ya kuchagua vyuo wanavyovyitaka, na kufanya Udahili wa papo kwa hapo.

Previous articleDP WORLD HAITAMILIKISHWA ARDHI YA TANZANIA.
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JULAI 17, 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here