Akizungumza kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara ya ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam AFISA Masoko wa shirika hilo Bw. Obadia Erasto amesema mfuko wa uwekezaji wa pamoja Faida Fund umekuja Kwa ajili ya kumkomboa mwananchi mmoja mmoja au vikundi kuwekeza Kwa maslahi Yao binafsi.
Amesema Faida Fund uwekezaji wake ni wa kiwango Cha chini Kwani uwekezaji wa awali ni shilingi elfu 10,000 wakati uwekezaji wa muda mrefu ikiwa ni shilingi elfu 5000.
Aidha Erasto amesema Mfuko wa Faida Fund unatoa fursa Kwa watanzania wa makundi na vipato mbalimbali,watumishi wa umma na wafanyakazi wa makampuni kuwekeza na kujiongezea vipato katika uwekezaji wa pamoja
Amesema mwekezaji atatakiwa kununua vipande vya kuanzia shilingi elfu 10 kupitia namba ya malipo itakayotumwa baada ya kujisajili katika mfumo ambapo baada ya hapo ataendelea kununua vipande Kwa kuanzia elfu 5.
“Mteja akija kuwekeza kwenye mfuko wa Faida Fund anakuwa anawekeza pesa taslimu” ameongeza Erasto
Aidha mauzo ya kuuza vipande vya mfuko wa Faida Fund yameanza tarehe 1.11.2022
Erasto ametoa Muongozo wa kujiunga na mfuko huo huku akitoa wito Kwa wananchi kujiunga ili waweze kunufaika na mfuko huo
ILI UWEZE KUNUNUA VIPANDE LAZIMA USAJILIWE KWANZA:
Jinsi ya kujisajili fuata utaratibu huu hapa chini:
1. Ingia kwenye menyu kuu ya Serikali kwa kubonyeza *152*00#
1. Chagua Malipo
6: Chagua WHI
1: Tengeneza akaunti ya binafsi
Ingiza majina yako kamili
Ingiza tarehe ya kuzaliwa: tar/meezi/mwaka.
Baada ya kuingiza tarehe ya kuziwa utapatiwa Namba ya Akaunti na Namba ya Malipo (Control Number)
Hivhyo sasa , baada ya kupata control number utaweza kununua vipande kwa kutumia Mpesa, au kwenda benki
Ikumbukwe kuwa malipo ya awali ni kuanzia 10,000/=
Baada ya kufanya malipo utapokea msg ya kuwa malipo yamepokelewaa na kisha msg ya kukupatia vipande vya uwekezaji.