NA HERI SHAABAN(ILALA)
JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala ina mikakati ya kujenga ofisi za Wazazi kila Kata .
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa JUMUIYA ya Wazazi Wilaya Ilala, Mohamed Msophe
Wakati akiwa Kata ya Minazi Mirefu Wilaya Ilala kukabidhi msaada cementi kwa ajili ya jumuiya hiyo.
Msophe alisema Mikakati yake ndani ya jumuiya hiyo kuijenga upya ikiwemo kuongeza wanachama wapya ndani ya Jumuiya sambamba na kukijenga Chama cha Mapinduzi
“Jumuiya ya Wazazi ni Jumuiya mama inalelewa na chama cha Mapinduzi mikakati yangu kuimalisha Jumuiya hii ikiwemo kujenga Ofisi za Wazazi na kujenga ofisi za Jumuiya yetu”alisema Msophe
Mwenyekiti Msophe alisema haiwezekani jumuiya ya wazazi waendelee kuishi kwa kupanga ofisi lazima wawe na mikakati ya kuwa na ofisi zao .
Aliwaomba viongozi wa wazazi kata kuweka mikakati ya kujiimarisha kiuchumi ikiwemo kuimalisha miradi ya Jumuiya hiyo.
Aliwataka makatibu Kata na Matawi kuongeza Wanachama sambamba na kuwa wabunifu kwa ajili ya kubuni miradi ya jumuiya kwa ajili ya kujiwezesha kiuchumi.
Wakati huohuo alifanya ziara yakutembelea kikundi cha wazazi majohe B na aliwaomba viongozi wote wa kata na matawi kuanzisha vikundi vya wanawake na walemavu wanaotokana na Jumuiya hiyo ili vipate mikopo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo aina riba juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Mwisho