Home LOCAL MWENYEKITI WAZAZI MSOPHE AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI KWA AJILI YA...

MWENYEKITI WAZAZI MSOPHE AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI KWA AJILI YA OFISI BUYUNI.





Na: HERI SHAABAN (ILALA)

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, Mohamed Msophe amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Wazazi za Jumuiya hiyo.

Saruji  hiyo alikabidhi Kata ya Buyuni leo kwa Mwenyekiti wa Wazazi Kata Ally Juma Wambanguru 

“Kampeni ya kujenga ofisi za Jumuiya ya Wazazi ni Kampeni yangu  endelevu kila Kata iwe na ofisi yake nikiwa Mwenyekiti wa Wazazi nitahakikisha nasimamia Jumuiya hii vizuri pamoja na chama” alisema Msophe

Msophe alisema mpango huo ni endelevu Wilaya nzima kuwa na ofisi ya Jumuiya kwa ajili ya kukisaidia chama na Jumuiya zake ziweze kufanya Kazi zake kwa ufanisi.

Msophe alisema Wilaya llala ina Kata 36 mpango wa ujenzi kila Kata iwe na Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi kwa ajili ya kulinda siri za chama na Jumuiya.

Mwenyekiti Msophe aliwataka viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kila Kata kuwa wabunifu kwa kubuni miradi mbalimbali ndani ya Jumuiya hiyo.

Msophe alisema Mikakati yake  kuijenga upya Jumuiya  ikiwemo kuongeza wanachama wapya ndani ya Jumuiya sambamba na kukijenga Chama cha Mapinduzi

Alisema Jumuiya ya Wazazi ni Jumuiya mama inalelewa na chama cha Mapinduzi  dhumuni  kuimalisha Jumuiya kifikie malengo yake sambamba na Chama cha mapinduzi .

Mwenyekiti Msophe alisema haiwezekani jumuiya ya wazazi waendelee kuishi kwa kupanga ofisi lazima wawe na mikakati ya  kuwa na ofisi zao .

Aliwaomba viongozi wa wazazi kata kuweka mikakati ya kujiimarisha kiuchumi ikiwemo kuimalisha miradi ya Jumuiya hiyo.

Aliwataka makatibu Kata na Matawi kuongeza Wanachama sambamba na kuwa wabunifu kwa ajili ya kubuni miradi ya jumuiya kwa ajili ya kujiwezesha kiuchumi.

Aidha aliwaomba viongozi wote wa kata na matawi kuanzisha vikundi vya wanawake na walemavu wanaotokana na Jumuiya hiyo ili vipate mikopo ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo aina riba kwa ajili ya kuunga mkono  juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Mwisho.

Previous articleSTARS KAMA MLIVYOSIKIA KATIKA MBIO ZA KOMBE LA DUNIA
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TATU NOVEMBA15-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here