Home SPORTS STARS KAMA MLIVYOSIKIA KATIKA MBIO ZA KOMBE LA DUNIA

STARS KAMA MLIVYOSIKIA KATIKA MBIO ZA KOMBE LA DUNIA

Mwandishi wetu.

TIMU ya Tanzania (Taifa Stars) leo  imekamilisha mechi zake za Kundi J kufuzu Kombe la Dunia kwa sare ya 1-1 na wenyeji, Madagascar jioni ya leo Uwanja wa Manispaaa ya Mahamasina Jijini Antananarivo.

Kikosi cha Taifa Stars kilitangulia kupata bao la mshambuliaji wa  Simon Happygod Msuva dakika ya 24, kabla ya mshambuliaji wa Lierse K ya Ubelgiji, Hakim Djamel Abdallah kuisawazishia Madagascar dakika ya 74.

Wenyeji, Madagascar walimaliza pungufu baada ya beki wa Saint-Pierroise ya Réunion, Pascal Razakanantenaina kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 83 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Msuva nje kidogo ya boksi.

Mechi nyingine ya Kundi J leo, wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Benin Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa.

Kwa matokeo hayo, DRC inamaliza kileleni kwa pointi zake 11, ikifuatiwa na Benin 10 na Taifa Stars nane, wakati Madagascar imeshika mkia kwa pointi zake nne.

Kongo inakwenda hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Qatar ambako itakutana na mmoja wa washindi wa makundi mengine tisa katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atakuwa mmoja kati ya wawakilishi watano wa Afrika Kombe la Dunia mwakani.

Previous articleRAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI
Next articleMWENYEKITI WAZAZI MSOPHE AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI KWA AJILI YA OFISI BUYUNI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here