Home BUSINESS NCHI 14 NA MAKAMPUNI  ZAIDI YA 1000 YATHIBITISHA KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA...

NCHI 14 NA MAKAMPUNI  ZAIDI YA 1000 YATHIBITISHA KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MWAKA HUU

DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imesema mpaka sasa tayari nchi 14 zimethibitisha kushiriki katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya kimataifa (DITF) maarufu Sabasaba.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo Mei 19,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa  TATRADE Fortunatus Mhambe amesema katika Maonesho hayo kuna mampuni ya ndani 1188  na mengine 112 kutoka nje ya nchi yamethibitisha kushiriki.

Amesema Maonesho hayo ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao na huduma wanazotoa sambamba na kutanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.

“Leo ningependa kuzungumzia kuhusu Sabasaba Expo Village ambayo ni moja kati ya programu za maonesho ya DITF. Eneo hili limejitolea kutangaza fursa zilizopo katika Sekta ya Madini, Tehama ,Gesi na Mafuta, siku ya mazingira, Sanaa, Vijana na Wanawake” 

Akifafanua zaidi Mhambe amesema kuwa katika Banda maalum la Sabasaba Expo Village, wajasiriamali watapata fursa ya kujionea na kujifunza mambo mbalimbali.

Expo Village itaweza kuonyesha uwezo wa ubunifu na uvumbuzi. Eneo hili linatoa fursa kwa wajasiriamali hasa vijanna na wanawake ,kuonyesha talanta zao na kushiriki katika shughuli za Biashara, hii  ni njia ya kukuza ujasiriamali na kuwapa fursa sawa wadau wote katika Sekta ya Biashara” 

Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara 2023 yanatarajia kuanza rasmi June 28, hadi Julai 13, huku yakiwa na  kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji’

Previous articleSERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WATENDAJI WANAOKWAMISHA JITIHADA ZA RAIS SAMIA 
Next articleTWCC YAWAITA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA (SABASABA) JIJINI DAR 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here