NA: HERI SHAABAN
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam wamezindua Usafi Wilaya ya Ilala ,kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya jiji.
Akizindua Kampeni ya Usafi ngazi ya Wilaya ya Ilala Meya wa Halmashauri hiyo Omary Kumbilamoto alisema Usafi ni jukumu letu sote kila mwananchi anatakiwa kufanya usafi katika maeneo yao kwa ajili ya kutunza mazingira.
“Leo tumezindua rasmi Kampeni ya Usafi ngazi ya Wilaya ya Ilala kata hii ya Vingunguti wiki hii yote ni mwendelezo wa kufanya usafi endelevu uzinduzi wa Usafi kwa Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 04/2021 kata ya Kivukoni Wilaya ya Ilala mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Amos Makala “ alisema Kumbilamoto.
Meya Kumbilamoto amewataka wananchi kujenga tabia ya kuwa wasafi katika maeneo yao kwa kusafisha mazingira na kufanya usafi kila siku .
Akizungumzia mikopo ya vikundi alisema halmashauri tayari wameshatoa zaidi ya Shilingi bilioni 6 vikundi vimekopa na mikopo mingine wanatarajia kutoa Mwisho wa Novemba mwaka huu katika Maonesho pale Viwanja vya Mnazi Mmoja .
Kwa upande wake Afisa Maendeleo Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Georgis Asenga, alisema katika madhimisho ya miaka 60 ya UHURU Idara ya Maendeo ya Jamii wanashiriki usafi na wananchi kwani usafi ni afya tujilinde katika maeneo yetu kwa kushiriki usafi.
Asenga alisema katika kampeni hiyo ya usafi wamefanya na vikundi mbalimbali vya kijamii,TASAF,Wajane wa Vingunguti na Changamka Mwanamke .
Mganga Mfawidhi Zahanati ya Vingunguti Chiku Simba alisema zahanati ya Vingunguti inatoa huduma bora kwa wananchi wa eneo hilo ikiwemo huduma za mama na Mtoto.
Aidha Daktari Chiku alisema pia katika Zahanati hiyo wanatoa chanjo ya COVID kwa wananchi wote asubuhi mpaka jioni.
MWISHO.